Ijue nchi ya uholanzi na vijimambo vyake

1. Ni nchi ya kwanza kugeuza eneo la bahari kuwa eneo la makazi (Land Reclamation)

2. Nchi Inayoongoza kwa kuwa na watu warefu zaidi duniani, wastani wa urefu wa wanaume ni sm 184 (karibu mita 2) ilihali wanawake ni sm 170

3. Nchi ya Kwanza Duniani Kuhalalisha Ushoga Mnamo Mwaka 2001

4. Nchi Yenye Idadi Kubwa ya Baiskeli Kuliko Hata Idadi ya watu, sensa ya mwisho inaonesha nchi hiyo ina Baiskeli milioni 18 sawa na zaidi ya baiskeli moja kwa kila raia

5. Nchi ambayo imehalalisha haramu nyingi kiasi cha kuwafanya watu wawe huru sana na hivyo kupunguza kama si kuondoa wafungwa kabisa. Hii ni nchi pekee ambayo imelazimika kuazima wafunwa toka mataifa mengine maana jela zao zipo tupu

6. Nchi ambayo wanawake hufurahia maisha kuliko nchi nyingine yoyote duniani kwa kupewa kipaumbele cha kwanza, wakifuatiwa na mtoto, Mbwa, Baiskeli na Mwanaume kipaumbele cha mwisho

7. Nchi yenye maduka ya ngono (sex shops) na vioski huru vya kuvutia bangi (maarufu kama coffee shops) ambapo unaingia na kuvuta bangi utakavyo kisha unarudi kitaa...yaani ukiingia coffee shop unakutana na menu za bangi tu

8. Miongoni mwa nchi maarufu kwa starehe duniani kwani licha ya kuongozwa kwa unywaji wa pombe yao maarufu ya Heineken pia inachagizwa na kauli mbiu ya S 3 (SAND, SUN AND SEX)

9. Nchi inayoongoza kwa unywaji wa kahawa duniani (wastani wa vikombe 3 kwa siku kwa mtu) sababu ni kwamba licha ya baridi kahawa inawafanya wasilale ili waendelee na starehe
The-feminismhappiness-axis.jpg
10. Likizo ya uzazi ni siku 57 na inaweza kuchukuliwa muda wowote hadi mtoto anapofikisha miaka 8!!

Post a Comment

0 Comments