Mfahamu J. Edgar Hoover kachero
aliyeogopeka zaidi katika historia ya
Marekani.
1. Jina lake halisi ni John Edgar Hoover
lakini alipenda kujulikana zaidi kama J.
Edgar Hoover. Ni Kachero aliyeheshimika na
kuogopwa zaidi ndani ya FBI na Marekani
kwa ujumla, ni mtu aliyekuwa na matukio
mengi ya kutatanisha.
2. Ndio muasisi wa Shirika la Upelelezi
nchini Marekani ( FBI ) baada ya kutoa wazo
la kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1935.
FBI ilianzishwa ikichukua nafasi ya Bureau
Of Investigation ( BOI ) ambapo J. Edgar
Hoover pia alikuwa ni Mkurugenzi wake
kuanzia mwaka 1924 mpaka 1935. Lengo la
kuanzishwa kwa FBI ilikuwa ni kuongeza
ufansi katika kupambana na uhalifu ndani ya
Marekani.
3. J. Edgar Hoover ndio Mkurugenzi wa
kwanza kabisa wa FBI akidumu kwenye
cheo hiko kuanzia mwaka 1935 mpaka 1972
alipofariki Dunia akiwa na miaka 77 ( Alifia
Madarakani ). Alidumu kama Mkurugenzi wa
FBI kwa miaka 32, hakuna Mkurugenzi
aliyekaa muda mrefu zaidi kama Hoover.
Jengo la Makao Makuu ya FBI limepewa jina
lake na linajulikana kama " J. Edgar Hoover
Building "
4. Katika miaka yake 32 kama Mkurugenzi
wa FBI, Edgar Hoover alihudumu kwa Marais
6 tofauti na hakuwa na mahusiano mazuri na
Marais hao. Marais hao ni Franklin D.
Roosevelt, Harry S. Truman, Dwight D.
Eisenhower, John F. Kennedy, Lyndon B.
Johnson na Richard Nixon. Rais Richard
Nixon aliwahi kusema alikaribia kumfukuza
kazi Edgar Hoover lakini alimhofia Hoover
angemharibia mambo yake ya kisiasa. Huku
Rais Harry S. Truman akisema Hoover
aliifanya FBI kama jeshi lake la siri.
5. Inasemekana Edgar Hoover aliogopwa
zaidi ndani ya Marekani kutokana na kuwa
na mafaili machafu ya watu maarufu na hata
Marais. Ndio maana Marais 6 katika vipindi
tofauti tofauti walishindwa kumfukuza kazi
wakihofia usalama wao zaidi. Mbinu
mojawapo aliyokuwa akiitumia Edgar Hoover
ni kurekodi mawasiliano ya Marais
waliokuwa madarakani na kutumia kama
kinga ya kujihami asitumbuliwe. Mfano Rais
John F. Kennedy alirekodiwa maongezi yake
ya kimapenzi na mrembo matata wa miaka
hiyo Marylin Monroe.
6. J. Edgar Hoover aliogopwa pia ndani ya
FBI kwani alitumia mbinu chafu katika
kuhakikisha hakuna mtu maarufu zaidi yake
ndani ya Shirika hilo. Mfano ni
kuwastaafisha kazi au kuwaua baadhi ya
maofisa waliokuwa wanataka kumzidi
umaarufu na kutishia usalama wa nafasi
yake kama vile Kachero Melvin Purvis
ambaye alisifika sana ndani ya FBI miaka ya
1930's kwa kudili na Majambazi. Lakini
Kachero Melvin Purvis aliacha kazi ghafla na
kufariki kifo tata.
7. J. Edgar Hoover alisifika kwa
kuwashughukia wahalifu wakubwa
waliovunja na kuiba katika Mabenki nchini
Marekani katika kipindi cha World Economic
Depression miaka ya 1930's. Baadhi ya
wahalifu sugu waliokamatwa au kuuwawa
kipindi hiko ni John Dillinger, Baby Face
Nelson, Pretty Boy Floyd na wengineo.
Pia inasemekana aliratibu baadhi ya mauaji
ya wanaharakati kama vile Martin Luther
King Jr.
8. J. Edgar Hoover hakuwahi kuoa, kuwa na
mwanamke wala kupata mtoto katika
maisha yake Duniani. Ni bachela wa muda
mrefu sana, na kuna tetesi ziliwahi kuvuma
kuwa ni shoga lakini hakuna aliyethibitisha
hilo. Kuna wanaosema kazi yake ilimfanya
awe bize zaidi na kusahau mambo ya
muhimu kama kuoa.
9. Mtu pekee Edgar Hoover aliyemuamini
katika shirika la FBI ni secretary wake bi
Helen Gandy. Mama huyu alikuwa ni mtu wa
karibu sana wa Edgar Hoover walifanya kazi
kwa pamoja kwa miaka 54 na ndiye
aliyekuwa anatunza siri nyingi za Edgar
Hoover. Kama ilivyo kwa bosi wake, Bi
Hellen Gandy hakuwahi kuolewa wala kupata
mtoto. Alichoma moto nyaraka muhimu za
bosi wake punde tu baada ya kifo chake
ikiwa ni sehemu ya kiapo chake. Alistafu
kazi ndani ya FBI siku moja baada ya kifo
cha J. Edgar Hoover.
10. Kwa kuhofia asije akajitokeza mtu
mwingine mwenye mawazo kama ya J.
Edgar Hoover, serikali ya Marekani kwa
kutumia Bunge lake ilitengeneza sheria ya
muda wa ukomo wa madaraka kwa
Mkurugenzi wa FBI, ambapo anatakiwa
asizidi miaka 10 madarakani. Kwani
walijifunza kutokana na Hoover kukaa
madarakani miaka 32 na kufanya shirika la
FBI kama mali yake hivyo kuwatesa Marais
wengi.
0 Comments