Mkwawa alikuwa chifu wa wahehe na kiongozi mkuu wa kabila la wahehe ambaye alizaliwa mwaka 1855 -1898 katika kijiji cha Lungemba mkoani Iringa.
Baba yake mzazi ni Mzee Munyigumba.Baada ya kuzaliwa Mkwawa alipewa jina la 'Ndasalasa' yaani ikiwa na maana ya kupapasa papasa. Alipoofikisha umri wa miaka 23 ulitokea uvamizi ambapo baba yake mzazi Mzee Munyigumba alivamiwa na Wangoni.
Baada ya kuvamiwa Mzee Munyigumba alikimbilia mlima wa Nyamulenge. Alipokuwa pale mlimani Wangoni walimzingira kila pande hivyo Mzee Munyigumba aliamua kuingia pangoni, baada ya kuingia pangoni Wangoni waliamua kuchoma moto pale pangoni ili basi Mzee Munyigumba afie ndani ya pangoni lakini mpango wao haukutimia kwani Mkwawa aliwahi kumuokoa baba yake.
Mzee Munyigumba alimsifu sana mtoto wake kwa ushujaa alioufanya wa kumkomboa hivyo alimtunuku jina la kishujaa yaani aliitwa "Mkwava Mkwavinyika".
Mapigano kati Mkwawa akiwa na wafuasi wake wa kabila la Wahehe dhidi ya Wangoni yalipamba moto sehemu ya Makambako ambapo Wangoni walishindwa na kuamua kukimbia.
Licha ya Wahehe kushinda lakini bado waliwasifu Wangoni kwa mapigano waliyoyaonesha wakisema kuwa " Leo tumekutana na Makambako" ikiwa na maana kuwa wamekutana na madume hivyo sehemu hiyo tangu siku hiyo ikawa inaitwa Makambako mpaka leo hii.
Lakini baada ya kumaliza mapigano dhidi ya Wangoni, Mkwawa na kikosi chake walirudi Iringa mjini. Kwa bahati mbaya alisikia taarifa mbaya kwamba baba yake amefariki hivyo ilibidi baba yao mdogo Mzee Mwaije agawanye nchi ambapo upande wa kusini alipewa Mkwawa na upande wa kasikazini alipewa Muhenga. Baada ya kupewa maeneo hayo Shemeji yao Mwambambe mwalinyungu ambaye asili yake ni mtu wa Tabora aliwagombanisha Mkwawa na Muhenga.
Mwambambe alifika Iringa wakati akiwa Mdogo sana hivyo baba yake Mkwawa alikuwa akimtumia kwenda kuchukua dawa za kichifu na dawa za kivita wakati wakiwa njiani pale walipotokea maadui Mwambambe alikuwa na nguvu za ajabu alikuwa na uwezo wa kumkamata adui mmoja kila upande na kuwagonisha vichwa mpaka wanafariki hivyo baba yake Mkwawa pamoja na wahehe wote kiujumla walimpenda sana Mwambambe kufuatia sifa hizo Mzee Munyigumba alimpatia binti yake amuoe. Hivyo Mwambambe aliwagombanisha Mkwawa na Muhenga kwa kumwambia Muhenga kwamba amepata eneo dogo kuliko Mkwawa hivyo alimwambia kuwa yeye yupo tayari kumsaidia ili apate eneo kubwa.
Wakaanzisha vita ya kumpiga Mkwawa hivyo Mkwawa alitoroka kuelekea Dodoma, wakati akiwa huko baba yake Mdogo aliyekuwa akiishi huko alimuuliza kuwa nchi kamuachia nani? Ilibidi Mkwawa amueleze kilichotokea na kumalizia kwamba amemuachia Mdogo, hapo ndipo baba yake Mdogo alipomwambia inabidi arudi Iringa kwa ajili ya kupambana kwani yule Mdogo wake pia anaweza kupigwa na Mwambambe akachukua nchi na Mwambambe asili yake ni mtu wa Tabora hivyo nchi itakuwa ya watu wa Tabora.
Basi ilibidi Mkwawa arudi Iringa kupambana na hao ndugu zake. Lakini kwa bahati mbaya hawa ndugu zake walishasababisha mauaji, walishinikiza mpaka mama yake Mkwawa alijiua. Baada ya Mkwawa kukimbilia Dodoma walimkamata mama yake na kumlazimisha awaoneshe dawa ya uchifu ambayo ilikuwa inaitwa "LIHOMEO" baada ya kuwa amelazimishwa sana mama Mkwawa aliamua kuwaambia kuwa dawa hiyo inapatikana sehemu inayoitwa Kikongoma hivyo waliondoka kuelekea huko Kikongoma kuchukua dawa. Walipofika Kikongoma walienda mpaka kwenye daraja la Mungu baada ya kufika hapo mama Mkwawa aliwaambia kuwa "Nimefika sehemu ilipo dawa lakini mashariti yake ni lazima nivue nguo ndipo niweze kuichukua hiyo dawa, sasa nyinyi ni wanangu nitavuaje nguo mbele yenu?" Hivyo wale jamaa ilibidi wawatume wamama wawili waende naye wao wenyewe walibaki nyuma kidogo.
Mama Mkwawa alisogea hadi karibu na daraja la Mungu sehemu ambapo kulikuwa na jiwe kubwa, mama mkwawa alivua nguo zake zote na kuziweka juu ya lile jiwe kisha akaanza kulizinguka lile jiwe Mara kadhaa halafu akajirusha ndani ya maji huku akisema, "Mwambambe ulitaka nikuoneshe dawa ili umuue mwanangu umenikosa". Alizungumza kwa lugha ya kihehe kisha akajirusha ndani ya ule mto.
0 Comments