Forojo Ganze Na Historia Ya Mwenge

Huyu Forojo Ganze,alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo,walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote(Mwl.Nyerere),zindiko hilo lilifanyika bagamoyo ktk moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo,zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee.Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia ktk hilo shimo kwaajili ya kuuliza,alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es salaam,kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika,wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno hayo
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl.Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru.
kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115,kisha akakata roho,baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani,baada ya hapo aliwagiza yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115.Kama kawaida ya shehe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38,hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115,na hii ndivyo ilivyokuwa,mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema,mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa bukoba jambo la kitaifa?,zindiko la bagamoyo linafanya kazi ,Safu hii ilikuwa ya watu 5 ambao ni. 1.mzee ramadhan,alizaliwa mwaka 1920,2.Ally tarazo(1929),3.Komwe wa Komwe(1918),4.Sheihe Yahya Hussein(1925),na 5.Forojo Ganze (1902)

Post a Comment

0 Comments