MJue Fela Kuti

Fela Olusegun Oludotun Ransome-Kuti alizaliwa 15-10-1938 katika mji wa Abeokuta, Mkoa wa Ogun, Nigeria. Fela alizaliwa katika famila ya kipato cha kawaida, mama yake Funmilayo Ronsome-Kuti alikuwa mpiganiaji wa haki za wanawake katika serikali ya kikoloni na baba yake Padre Israele Oludotun Ransome-Kuti, alikuwa padre wa kanisa la Anglicana, alikuwa mwalimu mkuu na alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Walimu. Kaka yake Fela Beko Ransome Kuti na Olikoe Ransome-Kuti wote walikuwa madaktari mashughuri nchini Nigeria. Binamu yake Fela ni mwandishi wa kwanza wa ki-Afrika aliewahi kupata tunzo ya Nobel kwa uwandishi wake Wole Soyinka.
 


Fela alikuwa mwanamuziki, mpiga tarumbeta, mtungaji wa nyimbo na mwanzilishi wa Afrobeat music genre, mpigania haki za binadamu na alitumia mziki kufikisha ujumbe wa siasa kwa jamii, mwana halisi wa Afrika ambae aliamini kwenye ndoa ya zaidi ya mke mmoja. Katika maisha yake atakumbukwa kama mwanamapinduzi mwenye kipaji cha mziki.

Fela alipata elimu yake katika shule ya Grammar ya Abeokuta mjini Abeokuta. Baadae alipelekwa London mwaka 1958 kusomea udaktari lakini aliamua kuacha masomo hayo na kusomea mziki Trinity College of Music, tarumbeta ikiwa kifaa alichopendelea zaidi. Akiwa chuoni Trinity Fela alianzisha bendi yake ya mziki iliyojulikana kama Koola Lobitos. Fela alimuoa mke wake wa kwanza mwaka 1960 ambae alipata nae watoto watatu (Femi, Yeni na Sola). Mwaka 1963 Fela alirudi Nigeria ambako aliendeleza bendi ya Koola Lobitos na alianza kujifunza kazi ya utangazaji wa redio ya Shirika la Habari la Nigeria. Alipiga mziki kwa muda na Victor Olairy pamoja na bendi yake ya All Stars.

Mwaka 1977, Fela na bendi yake ya Afrika '70 walitoa album ya Zombie, ikiwa ni shambulio kwa serikali ya Nigeria alitumia neno la zombie kuelezea mbinu za askari na wanausalama wa Nigeria. Album hii iliuzika sana na ilileta tafrani katika serikali na ilipelekea kuanza kwa shambulio la Kalakuta Republic, (hii ilikuwa Republic ilianzishwa na Fela) katika shambulio hilo maelfu ya askari walijeruhi raia. Fela alipigwa sana na mama yake ambae alikuwa mzee (ambae nyumba yake ilikuwa mbele tu ya eneo la fujo) alirushwa dirishani, kitendo hicho kilimsababishia majeraha makubwa. Kalakuta ilichomwa moto na studio za Fela pamoja na vyombo vyake vya mziki viliharibiwa. Fela alinukuliwa akisema ilikuwa auwawe katika vurugu hizo kama si amri ya Afisa Usalama mmoja aliyeingilia wakati anapigwa. Fela alitakiwa kupeleka jeneza la mama yake Dodan kwenye himaya ya Generali Olesegun Obasanjo na alitakiwa kuandika nyimbo mbili "Coffin for Head of State" na "Unknown Soldier" ikimaanisha kuwa mashambulio yalifanywa na askari asiyejulikana.

Fela na bendi yake walihamia Crossroads Hotel, baada ya eneo la makazi na shughuli zake kuharibiwa vibaya. 1978 Fela alioa wanawake 27, wengi wao wakiwa wachezaji katika bendi yake, hii ilikuwa katika kumbu kumbu wa mwaka mmoja baada ya shambulio la makazi yake Kalakuta Republic. Baadae alianzisha mtindo wa kuwa na wake 12 tu. Mwaka huo alifanya maonyesho makubwa mawili mjini Accra na fujo kuwa zilitokea wakati mziki wa Zombie ulipopigwa. Hii ilisababisha Fela kupigwa marufuku kuingia nchini Ghana.

Mwaka 1984, serikali ya Muhammadu Buhari ilimtia hatiani Fela kwa kosa la kutorosha fedha, kosa ambalo Amnesty International ilithibitisha kuwa ilikuwa ni mbinu za kisiasa. Amnesty iliweka kesi hii katika daraja la mfungwa wa kisiasa na ilisimamiwa na vikundi vya utetezi wa haki za binadamu. Baada ya miezi 20 jela, Fela aliruhusiwa kutoka gerezani na Generali Ibrahimu Babangida. Alipotoka jela aliwapa talaka wake zake wote12 na alinukuliwa akisema "ndoa inaleta wivu na ubinafsi".

Mnamo tarehe 03-08-1997 Olikoye Ransome-Kuti ambae alikuwa katika mstari wa mbele katika matibabu na uelimishaji wa ugonjwa wa AIDS akiwa Waziri wa Afya, alitangaza kifo cha mdogo wake kuwa kilisababishwa na AIDS. Zaidi ya watu milioni mbili walihudhuria mazishi ya Fela. Baada ya hapo, mtoto wake Femi Kuti ameendeleza makazi ya Afrika Mpya yaliyoanzishwa na baba yake nje kidogo ya mji wa Lagos.

Post a Comment

0 Comments