Arianda Grande atagharamia mazishi ya watu 22 waliofariki kwenye shambulio la bomu kwenye show yake.

Baada ya kufuta show zake saba zilizobaki kwenye ziara yake ya Dangerous Woman pop staa kutoka Marekani Ariana Grande amewasiliana na familia za wafiwa wa bomu lililolipuka kwenye show yake Manchester ili kutoa msaada wowote kwenye mazishi ya ndugu zao.
Ariana amejitoa kugharamia mazishi ya watu 22 waliofariki kwenye show yake katika ukumbi wa Manchester Arena
Mpaka sasa polisi wanasema kijana aliyejilipua kwenye show ya Ariana Grande ni Salman Abedi na hakufanya tendo hilo mwenyewe, kuna mtandao mkubwa wa magaidi nyuma yake.

Post a Comment

0 Comments