Pop staa Taylor Swift amekuwa mafichoni kwa muda wa miezi mitatu sasa na imegundulika alikuwa studio akitaarisha album yake mpya.
Pia taarifa mpya ni kuwa Taylor Swift ana mpenzi mpya anayetokea Uingereza. Gazeti la #TheSun kuwa Taylor Swift yuko kwenye mahusiano na mwigizaji Joe Alwyn na kwamba Bi Swift hataki waandishi wa habari na mapaparrazi kujua kuhusu mahusiano yake kwa sasa.
Taylor na mpenzi wake wamekuwa walitumia ndege binafsi kwa muda mrefu ili kukaa mbali na mapaparrazi.
Taylor alikimbia macho ya watu baada ya mahusiano yake na DJ Calvin Harris kuvunjika na baadae kutoka na Tom Hiddleston kwa muda mfupi.
0 Comments