Billnass; Kufanya muziki na chuo nimepoteza pesa nyingi sana

Msanii Billnass ambaye pia ni mwanachuo CBE Dar es salaam ameongelea pesa alizopishana nazo wakati yupo masomoni nakudai alibidi aweke pembeni show ili kupiga kitabu.
Billnass anasema “Kufanya muziki na chuo nimepoteza pesa nyingi sana, watu wengine hawawezi kujua, nimeshakataa ‘show’ nyingi sana, nimeshaacha kwenda kwenye matamasha kibao…Vitu vingi sana vya kimuziki vilinipita na ndiyo ilikuwa ‘time’ yangu, kipindi cha ‘Chafu pozi’ inawika nilikuwa napata dili nyingi sana yaani hela ambayo najua kabisa hata nikimaliza chuo nisiweze kuitengeneza lakini masomo yalinibana zaidi“. 
Billnass akiwa shule ameweza kutoa hits kubwa kwenye radio na tv kama Raha na Chafu Pozi.

Post a Comment

0 Comments