Ndege ya Samaritans Purse iliyochukua watoto wa Lucky Vicent imewasili Marekani


Mnamo May 14, 2017 Ndege ya Samaritans Purse iliondoka Tanzania kwenda Marekani kwaajili ya kupeleka watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya basi la Lucky Vicent ili kupata matibabu nchini Marekani.
Leo May 15 Mh LazaroNyalandu amedhibitisha kuwa ndege hio imewasili Marekani salama na watoto watapelekwa kwenye hospitali ya Mercy mjini Sioux kwenye jimbo la Iowa kwaajili ya matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa Post ya Mbunge Lazaro Nyalandu inasema >>Ndege iliyochukua watoto wetu KIA jana imewasili Mjini Charlotte NC, nchini Marekani saa moja iliyopita (majira ya saa 3 asubuhi, saa za Afrika ya Mashariki). Watoto wamepelekwa Moja kwa Moja hospitali kuu mjini Charlotte kwa ajili ya kuimarishwa kiafya (medical stabilisation), na baadae watachukuliwa kwa ndege nyingine maalumu (air ambulance) kuelekea hospitali ya Mercy, Iliyopo Sioux City, katika Jimbo la Iowa kwa huduma kamili za matibabu” …
Tunawatakia matibabu mema watoto hawa, Mungu Awajalie Zaidi….

Post a Comment

0 Comments