Mwamuzi wa bao la Mkono la Maradona afariki dunia

Mwamuzi msaidizi kutoka nchini Bulgaia Bogdan Dochev, aleshindwa kuona bao la Mkono la mchezaji wa taifa wa Argentina, Diego Maradona wakati wa mchezo wa fainali za kombe la Dunia mwaka 1986 kati ya timu hiyo na Uingereza amefariki dunia.
Mchezaji wa Timu ya Taifa  ya Argentina, Diego Maradona(kushoto) akipiga mpira kwa Mkono kuelekea golini mwa Uingereza(kulia) golikipa wa Uingereza akijarabu kuokoa  

Mwamuzi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 80, anakumbukwa zaidi katika mchezo huo wa robo fainali Argentina ilishinda jumla ya mabao 2 kwa 1, huku Maradona akifunga mabao hayo yaliobaki katika historia ya Soka Duniani.
Baada ya kufunga bao la kwanza kwa Mkono lililopewa jina la ‘Goli la Mkono wa Mungu’, Diego Maradona alifunga bao la pili kwa kuwalamba chenga wachezaji watano wa Uingereza na kisha kutumia nafasi hiyo kufunga goli lake la pili katika mchezo huo.
Mchezaji wa Timu ya Taifa  ya Argentina, Diego Maradona(kushoto) akipeana Mkono na  golikipa wa Uingereza .
Lilipoingia bao la Mkono picha za runinga zilimuonesha mwamuzi raia wa Tunisia Ali Bin Nasser, akikimbia taratibu kuelekea katikati ya Uwanja huku akimtazama Dochev, kama atamuonesha kitu chochote lakini Mbulgaria huyo alikaa kimya kuashiria goli.
Baada ya mchezo Dochev alisema”Diego Maradona atasalia katika maisha yangu. Nimchezaji mwenye kipaji lakini ana mwili mdogo”.
Bogdan Dochev, aleshindwa kuona bao la Mkono la mchezaji wa taifa wa Argentina, Diego Maradona fainali za 1986, Argentina na Uingereza 
“Japokuwa nilihisi kuna jambo halikuwa sawa, lakini wakati ule Fifa ilikuwa hairuhusu Mwamuzi msaidizi kujadiliana lolote na mwamuzi wa kati”, aliviambia vyombo vya habari vya Bulgaria

Post a Comment

0 Comments