Fergie aikacha Black Eyed Peas

Mwanamuziki kutoka kundi la The Black Eyed Peas lililopo Marekani, Fergie, hatimaye ameamua kukusanya mikoba yake na kulikacha kundi hilo.
Kundi la Black Eyed Peas


Tangu  mwaka jana kulikuwa na tetesi kuwa Fergie ameachana na kundi hilo, Kauli ya will.i.am imethibitisha hilo wakati wa mahojiano na Ahlan! siku ya jana.


Fergie


”Hakuna mtu yoyote aliyechukua nafasi ya Fergie tangu aondoke, ila kwa sasa anafanya kazi zake binafsi”amesema will.i.am ambaye wanasherekea miaka 20 tangu kuanzishwa Black Eyed Peas .Hata hivyo will.i.am amekanusha taarifa zilizokuwepo kuwa msanii Nicole Scherzinger kujiunga na kundi hilo, bali ameeleza kuwa msanii huyo wanafanya naye projeti tu .
”Nicole kwa sasa nafanya projecti na sisi(kundi) ila sitaki kusema sana kuwa tunafanya kitu gani na yeye” amesema will.i.am
Kundi la Black Eyed Peas lilianzishwa mwaka 1998, na kutambulika rasmi mwaka 2000 kisha Fergie kujiunga na kufanya kazi ya kwanza “Elephunk”,na baadae kuendelea kufanya kazi kama vile Monkey Business(2005), The E.N.D.(2009) na The Beginning(2010).

Post a Comment

0 Comments