Sehem ya 2; Maneno Kutoka Kwa Wananchi Jinsi Ilivyokuwa Siku Ya kifo cha Dr wilbert kleruu

Kutoka Iringa mjini Kleruu ameamua kwenda Isimani bila ya mlinzi/dereva. Ikumbukwe pia ameshakuwa very unpopular na wanyalukol o na word was out kuwa yeyote atakayempata kwanza ammalize (haya ni maneno ya wanyalukolo wa enzi hizo) Alipopita kwa Mwamindi na akamuona Mwamindi yupo shambani kwake ndipo akamfuata huko huko na kuanza kumkejeli. Inasemekana Kleruu alikuwa ana kifimbo kama kile cha Mwalimu na akaanza kumchomachoma kifuani Mwamindi huku akimwambia"wewe nani kakupa ruhusa kulima jumapili? Si ulitakiwa kulima kwenye shamba la kijiji cha ujamaa tuu?" etc etc.

Mwamindi akaingia ndani akachukua shot gun yake(nadhani ilikuwa zile wanaziita two-two rifle, popular sana enzi hizo) na akatokea kwa nyuma (nyumba za waHehe zina mlango/dirisha mdogo kwa nyuma) na akamtwanga risasi na kikafuata kilichoelezwa hapo juu. Ila alipofika Iringa alikwenda kwanza kwa wake zake na kuwaambia alichofanya ndipo akaenda police station. Kuna mzee mmoja alipishana na Land Rover ya Kleruu na akashangaa kumuona Mwamindi anaendesha, na hapo hapo akajua soo limetokea, akapita shambani kwa Mwamindi na akaelezwa kilichotokea. Vilevile, kule mtaani watu walishangaa Mwamindi anaendesha kari la mkuu wa mkoana limepaki kwake! Waliokuwa wanajua walielewa mara moja nini kimetokea!

Post a Comment

0 Comments