Mambo Ma 5 Usiyoyajua Kuhusu Freddie Mercury

 

Freddie
Mercury alizaliwa King Stone Zanzibar na kukulia visiwani humo kabla ya Wazazi
wake kuhamia India na baadaye Middlesex England Freddie aliyezaliwa mnamo 05 mwezi Septemba mwaka 1946 alifariki akiwa
na umri wa miaka 45 mnamo tarehe 24 mwezi Novemba mwaka 1991


TWENDE MOJA KWA MOJA KWENYE MAMBO
YETU MATANO
5. Freddie Mercury alikuwa na uwezo
usio wa kawaida katika mpangilio wa sauti... yani uimbaji
Uongeaji
wake ulikua kwenye baritone, lakini uimbaji wake mwingi ulianguka katika kiwango
cha tenor. Mnamo mwaka 2016, timu ya wanasayansi iliamua kusoma sauti ya
Mercury. Miongoni mwa mambo waliyoyathibitisha  ni kwamba kamba za sauti za Mercury zilisonga
haraka kuliko mtu wa kawaida. "Wakati vibrato ya kawaida hubadilika  kati ya 5.4 Hz na 6.9 Hz, Mercury ilikuwa 7.04
Hz," Matokeo ya Sauti yaliripoti.

4. Freddie Mercury alipenda sana paka.

Alipenda sana
paka hadi aliwafuga paka kumi sehem moja. Aliwahi toa album inayoitwa (Mr.
Bad Guy
) ambamo ndani yake aliandika kibao alichomdediketia nyau wake
mpendwa Delila

Icheki kidogo

Delilah, Delilah, oh
my, oh my, oh my - you're irresistible

You make me smile when I'm just about to cry

You bring me hope, you make me laugh - you like it

You get away with murder, so innocent

But when you throw a moody you're all claws and you bite -

That's alright !

Delilah, Delilah, oh my, oh my, oh my - you're unpredictable

You make me so very happy

When you cuddle up and go to sleep beside me

And then you make me slightly mad

When you pee all over my Chippendale Suite

3.
Inaripotiwa ya kwamba Freddie Mercury alikua na aibu iliyopitiliza.
Licha ya kutambulika kuwa ni mtu mwenye fujo nyingi
jukwaani, watu wengi waliomtambua kwa maisha ya kawaida wanasema alikua ni mtu
mwenye aibu nyingi nah ii ndio sababu ya yeye kutoonekana kwenye interview
nyingi kama walivyokua ma star wengine. Katika maisha ya kawaida hakuna
anayemfaham Freddie (mshirika
mwenzake wa kwenye band
Roger Taylor aliwahi kusema) Alikua mwenye aibu
na mstaarabu. Hajawahi kuwa Yule anayeonekana stejini
.

2. Microphone isiyoishia chini (iliyo nusu almaarufu kama
"bottomless mic" ilikua ndo bidhaa yake kubwa nahii ilipelekea kupata
wateja wengi pia wa aina hii ya mike.

Mwanzoni kabisa
mwa kundi la queens, Freddie na wenzake wakiwa stejini. Stand ya mike ya
Freddie ilichomoka na kubaki kipande lakini chaajabu hakubadilisha microphone
na ukawa ndio mwanzo way eye kuanza kutumia microphone fupi.

1. Freddie Mercury aliwahi kuwa mpakiaji na mbeba mizigo
katika kiwanja cha ndege cha Heathrow.

Mwanzoni kabla
hajawa msanii maarufu Mercury aliwahi kuwa kwenye kitengo cha mizigo katika Heathrow
Airport. Katika kusherehekea miaka 72 toka azaliwe Freddie, Baadhi ya
wafanyakazi wa British Airways kitengo cha mizigo waliwaburudisha abiria kwa
kuvaa na kujiweka kimwonekano wa Freddie huku wakiimba na kucheza kwa
kumkumbuka mfanyakazi mwenzao.

 

Ahsante sana,
mimi ni Humphrey Moris, usisahau kusubscribe channel yangu,kucomment na kushare
sehem mbalimbali bila kusahau kupitia video zilizopita na kubonyeza alama ya
kengele ili kuziona video zinazofuata bye bye

Post a Comment

0 Comments