Edsheeran Awaonyesha Watanzania Wanaopendana Katika Video Yake Mpya (PUT IT ON ME)


Msanii maarufu kwenye mtindo wa Pop kutoka nchini uingereza Edward Christopher Sheeran almaarufu kama Edsheeran. Ametoa video mpya inayozungumzia watu wanaopendana kwa majimbo na baadhi ya nchi.

 

 Kwa upande wa Tanzania aliwaonyesha wa Australia wawili kwa majina ya Stephanie na Tyson ambao wametembelea Zanzibar kwaajili ya honeymoon wiki mbili baada ya ndoa yao.

Pia akawaonyesha wengine ambao ni Nasri na Khadija waliofunga ndoa mwaka 2009 wakifurahi huku wanacheza muziki. Kwa upande wa bara amewaonyesha Esther pamoja na David wakiwa wameshafunga ndoa miaka mi tatu sasa, Wanaonekana wakiwa na furaha.




Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii wakubwa kutaja au kuwaonyesha watanzania kwenye video zao. Msanii mwingine maarufu kwa jina la PASSENGER, kwenye video yake ya wrong direction amemwonyesha mwanariadha wa Tanzania akiwa amevaa jezi ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments