Katika maandiko yangu yote na huu mfumo wangu wa kutengeneza jarida la
historia za sehemu/watu mbalimbali, Bibi Hellen nimempa nafasi kubwa. Sijawahi
onana naye ila nimejaribu kukusanya baadhi Ya data zinazomuhusu.
Anastahili kuwa shujaa.
Dk Kijo-Bisimba amekuwa Kinara wa harakati za haki za binadamu nchini
Tanzania , akiwa kama mlinzi wa haki za binadamu kwa muda mrefu amekua mwenye
ushawishi mkubwa na kuwa chachu ya vijana wengi wachanga kuingia katika uwanja
wa sheria kwasababu yake.
Alizaliwa mnamo mwaka 1954 katika mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
Morali ya kuwa mwanaharakati aliipata miaka ya 1970 akiwa mwanafunzi katika
shule ya Korogwe huko Tanga. Baada ya walimu kumtuhumu kuwa alimwandikia barua
ya kumchafua mkuu wa shule hiyo. Mama Bi Simba, alijiudhulu nafasi yake ya dada
mkuu msaidizi na kupewa adhabu ya kukaa nyumbani kwa muda. Baba mzazi wa Bi
SIMBA alimwombea msamaha lakini walimu hawakukubali mpaka pale alipoomba
mwenyewe msamaha kwa kukiri kosa ambalo hakulitenda.
“Niliadhibiwa kosa kubwa ambalo sikulitenda ningali
dada mkuu msaidizi, kwanini hawakuniamini kuwa sikufanya kosa hilo licha ya wao
kuniamini mimi kuongoza kama dada mkuu msaidizi”
Mwaka 1996, Bibi Hellen alikua ni moja ya viongozi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na akiwa kama mmoja wa waanzilishi. Alitakiwa kuchukua nafasi ya
ukurugenzi na kuwa na jukumu la kutetea
masuala ya jinsia, rangi na dini, Anasema kwake ilikua ni kazi ambayo aliipenda
kwa moyo wake wote. “Niliipokea nafasi
ile ii niwatumikie watanzania”. Anasema hata watoto wake wanne huishi na
kujiamini kwa kumtazama mama yao akiwa kama mama mchapakazi. “Nimekuwa mjane toka mwaka 1994 lakini
watoto wangu ni imara na wanafanya kazi zao kama ninavyowajibika mama yao.
Kabla hajajiunga na LHRC , Dr Hellen alikua mwalimu wa kingereza na
kiswahili katika taasisi ya elimu ya watu wazima. Ambapo alifanya kazi kwa
miaka 10. Alihamasika kusoma sheria kutoka kwa marehem mumewake na wakati
alipoanza kufanya kazi LHRC alikua bado anajitolea katika shirika la wanawake
katika sheria na maendeleo barani afrika WILDAF. Ni shirika ambalo
aliliwakilisha katika mkutano wa kimataifa wa Beijing katika maendeleo ya
wanawake mwaka 1995.
Mwaka 2001, Dr Kijo Bisimba alisimama kama mwanamke wa kwanza kutoa
tamko la kuipinga serikali baada ya wananchi kuuawa huko Zanzibar kwasababu ya
mgogoro wa kisiasa. Ujasiri huo ulimpelekea kupata tuzo akiwa kama mwanamke wa
kwanza kutoka nchini Tanzania , kupata tuzo ya Woman of Courage ambayo
ilitolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 2008. Bibi Hellen
anasema, “kila mtu ana haki ya kuishi hata kama akiwa ni mkosaji”
Mwaka 2008-2011 alichukua mapumziko kwaajili ya kusoma PHD
nchini uingereza na kumfanya kuwa mmoja kati ya wanawake wa chache nchini Tanzania
kuwa na PHD haswa kwenye suala la haki za binadamu pamoja na sheria. Research
yake ilijikita kwenye masuala ya haki za watoto. KWANINI HAKI ZA WATOTO? “Nimetaka kuwapatia watoto wa kiafrika sauti
na kuona ni namna gani wanautazama mfumo wa serikali katika nchi, na ninadhani
kuelewa na kuwatambua watoto ni msingi
mzuri wa baadae kwa serikali” anaongeza kwa kusema “ watoto wa leo ndio
viongozi wa baadae” Dr Hellen.
"Ni mama mzuri ambaye anafanya lile analolihubiri na hakuna
kinachoweza kumstopisha pale anapohitaji kufanikisha jambo" Alisema
Mwalongo ambaye alifurahishwa na upendo wa Dr Hellen kwa watoto ambapo licha ya
kuwa mjane, bado anatunza watoto wasio na wazazi (yatima) nyumbani kwake na pia
ni memba wa umoja wa wasio na wazazi katika kanisa lake.
26 june 2012 Mida ya usiku aliwahi kupigiwa simu na
madaktari ambao walikua kwenye mgomo na kumpa taarifa ya kupotea kwa mwenzao
Dr Stephen Ulimboka, alishangazwa na
kushtuka kwakua hakutambua kosa lake zaidi ya kupambana kwa maslahi yao wao
kama madaktari
Alikaa na madaktari na kuitaka serikali kufanya uchunguzi na kumjua ni
nani alikua nyuma ya tukio hili la kinyama na kuhakikisha sheria inafuata
mkondo wake. Hili sio tukio pekee lililowahi kumkuta mama huyu kwaajili ya
kupambania haki.
Mwaka 2018, Dr Hellen, alikemea vikali kama mzazi tulio la mwanafunzi wa
chuo kikuu cha usafirishaji Dar es Salaam (NIT)
ambaye alifariki baada ya kupigwa risasi ya kichwa kimakosa na afisa wa
polisi aliyekuwa anajaribu kutuliza ghasia za waandamanaji wa kisiasa wa CHADEMA mnamo tarehe 16 Februari siku ya Ijumaa, 2018 huko Kinondoni.
Mnamo mwaka wa 2019 Waziri wa Mambo ya Ndani wa muda huo nchini
Tanzania Kangi Lugola alisema kuwa anashindwa kuelewa ni kwanini Kijo-Bisimba
hajatunzwa na nchi yake.
Lugola Aliyasema hayo alipofungua ofisi ya Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu siku ya alhamisi ya tarehe 26 Septemba 2019.
Ni mfano wa kuigwa pale linapokuja suala la
kutetea haki za binadamu kwenye nchi yake. Alikua anaamini na nadhani mpaka
sasa anaamini katika usawa wa haki za binadamu. Kusema ukweli sijui ni kwanini
hajapewa tuzo kwenye nchi yake. Alisema Kangi Lugola.
Dr Hellen Kijo Bisimba ametumikia kituo cha
sheria na haki za binadamu toka mwaka 1995 mpaka alipostaafu mwaka 2018.
Dr Hellen anaamini ya kuwa, Tanzania ni nchi nzuri na ya amani, ila kuna
baadhi ya mambo yanajitokeza sasa yanaweza kuleta matatizo makubwa hapo baadae.
Anasema suala la ukabila na udini ni mambo yanayojitokeza kwa kasi sasa wakati
zamani hayakuwapo. "Ninaamini hii ni changamoto ambayo serikali inapaswa
kuifanyia kazi, ili ncho yetu iendelee kujivunia amani na umoja ambao
tunao" Dr Hellen
0 Comments