HISTORIA:TOM MBOYA, AFRIKA NA UAFRIKA VOL 1


Kwa wapenzi wa muziki, kibao cha Nerea kilichoimbwa na Saut Soul, dakika za mwishoni anatajwa Tom Mboya. Ni kawaida kwakua nyimbo hii imewataja mashujaa wengi wa Afrika.
Nyimbo nyingine ya SAUT SOL FT NYANSHISKI, Tujiangalie, kuna sehemu wanasema
Wanamuziki wa kikundi cha Saut Sol kutoka KENYA


Na TOM mboya ameshika tama
Alituacha kama angali kijana 
Je angekuwa mambo yangekuwa sawa?
Ndivyo alivyopanga maulana
Kama nimekosea ntarekebishwa. Ametajwa tena TOM MBOYA

 Karibu umjue mboya kwa machache kwamaana mengi aliyoyafanya hayawezi andikika.
Mboya, ambaye jina lake kamili ni Thomas Joseph Odhiambo Mboya, alikuwa ni mmoja wa waasisi wa Chama cha Kenya African National Union (Kanu) kilichotawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1963.


Alisoma na kupata elimu ya juu, akaenda Uingereza na kurejea nyumbani mwaka 1956 akafanya kazi na baadae akajiunga na siasa. Wakati huo Waingereza walikuwa wanajaribu kulidhibiti wimbi la wapigania uhuru wa Mau Mau, waliokuwa wanataka ardhi yao na uhuru wa Kenya. Mungu nipe uhai siku chache zijazo niweke uzi wa Marehem Dedan Kimathi, mpiganaji na kiongozi wa vita vya maumau.
Mboya Aliingia katika bunge ambalo miongoni mwa wabunge 50, Waafrika walikuwa nane tu.
Akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa All-African Peoples Conference nchini Ghana, kwenye mkutano ambao uliitishwa na Kwame Nkrumah. Wakati huo Mboya alikuwa na umri wa miaka 28.



Mnamo1959, alianzisha mchakato wa kupeleka Waafrika kusoma nchini Marekani, ambapo wanafunzi 81 walihusika.
Juhudi hizo za Mboya zilimfanya Rais John Kennedy wa Marekani mwaka 1960, kujumuisha pia wanafunzi kutoka Uganda, Tanganyika (Tanzania) na Zanzibar, Rhodesia ya Kaskazini (ambayo sasa ni Zambia) Rhodesia ya Kusini (sasa ni Zimbabwe) na Nyasaland ambayo sasa ni Malawi.
Mradi huo uliwezesha wanafunzi 230 wa Afrika kupata masomo nchini Marekani mwaka 1960 ambapo mamia zaidi walifuatia mwaka 1961.



Barack Obama Sir, baba wa Barack Obama ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mboya . Naye pia alipata bahati ya kwenda kusoma Marekani kupitia mchakato huo. Labda bila mboya leo hii, tusingekuwa na Barack Obama, unadhani baba yake angempatia wapi yule binti wa kizungu? Tuachane na hayo.
Baba mzazi wa Barack Obama akiwa na mwanae Barack Obama
 Ni katika Mtaa wa Independence Avenue (ambao sasa ni Moi Avenue), mchana wa Julai 5, 1969 ambapo Nashon Isaac Njenga Njoroge alimpiga risasi na kumuua Mboya akiwa anatoka katika duka moja la madawa.

Mboya, aliyekuwa na umri wa miaka 39, alikufa papo hapo.
Baada ya kukamatwa kwake, Njoroge alisikika akisema: Kwa nini hamuendi kumuuliza bwana mkubwa?
Mtu huyo aliyeitwa bwana mkubwa kamwe hakufichuliwa, jambo ambalo linaaminika mpaka leo kwamba Mboya aliuawa baada ya kuonekana angekuwa tishio kwa rais wa nchi hiyo. Inasadikika lakini, siyo mimi niliyesema maneno haya.


Hatutawahi kamwe, kuuza uhuru wetu kwa mtaji au misaada ya kiufundi. Tunapigania uhuru kwa gharama yoyote. Tom, Mboya

Post a Comment

0 Comments