NA #Twitreporter
Nimeandika hii, kwaajili ya kuwapatia watu picha kamili kwa lengo la
kukujuza / kuelimisha / Kwa wengine ni burudani pia. Sina lengo la
kuchonganisha, wala kubagua
Kuuliwa kwa Malcolm X
Mnamo
Februari 21, 1965, Malcolm X aliuawa wakati akitoa hotuba katika ukumbi
wa Audubon Ballroom huko New York City. Aliuawa mbele ya familia yake.
Watazamaji wenye hasira wakamshika na kumpiga mmoja kati ya wahusika wa
mauaji hayo, ambaye alikamatwa kwenye eneo la tukio. Mashuhuda wa macho
waliwagundua watuhumiwa wengine wawili.ambao walikuwa wanachama wa
jumuia ya kiislam (NOI), walihukumiwa kifungo cha maisha jela.
Wajumbe watatu wa Taifa la Uislamu (NATIONAL OF ISLAM (NOI)) - Talmadge Hayer au Thomas Hagan (aka Mujahid Abdul Halim), Norman Butler (aka Muhammad Abdul Aziz) na Thomas Johnson (aka Khalil Islam) - walitiwa hatiani kwa mauaji yake mnamo 1966. (NATIONAL OF ISLAM
(NOI)) ni asasi ya kidini na kisiasa ya wamarekani wenye asili ya
Kiafrika iliyoundwa mnamo 1930 ikiwa na lengo la kuboresha hali ya
kiuchumi na kiroho kwa jamii watu weusi huko Marekani. Malcolm X
alijiunga na kikundi hicho mnamo 1952.
Malcom
x alizaliwa Omaha nchini Marekani kwenye familia ya baba mchungaji na
mwanaharakati wa haki za watu weusi ambaye aliishi kwa falsafa za Marcus
Garvey. Baba wa Malcom alifariki kwa kinachosemekana kuwa ni ajali ya
gari, lakini ilifahamika kuwa aliuawa na kikundi cha kudhibiti harakati
nchini Marekani KHU KLUX KLUN. Wakati huu Malcom alikua na miaka 6. Yeye na ndugu zake waliishi maisha ya kuhama hama na ndio sababu ya elimu yake kusuasua
( Ndoto yake alitamani kuwa mwanasheria) lakini mwalimu mzungu alimwambia WE UMESKIA WAPI KUNA MTU MWEUSI MWANASHERIA?..
akaacha na shule yenyewe akaingia mtaani kujiunga na masela. Mguu shoka
mkono upanga ukipita mbele yake anakukwapua. Mwisho wa siku miaka ya
1940 aliswekwa jela kwa kosa la udokozi, uvunjaji na kuvamia majumba ya
watu ili kujitaftia riziki (MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE)
Akiwa jela alisilimishwa (alibadili dini) na kuwa muislam . 1952 ALITOKA JELA AKIWA KIJANA MPYA. Na kujiunga (NATIONAL OF ISLAM
(NOI)) na ghafla alionekana kuwa mtu muhimu sana kwenye jumuiya ya
waislam. Kwakua alikua na uwezo mkubwa wa kuongea. Falsafa ya Malcom
haikua kutia vurugu bali ni kujilinda (self defense)
NI KITU GANI HASA KILISABABISHA KIFO CHAKE?
MWAKA
1964 Malcom alijitoa kwenye chama cha waislam kwakua hakuelewa nini
hasa dhamira ya kiongozi wake ELIJAH MOAHMED. Kulikua na mambo kadhaa
yanaendelea kwa jamii ya waislam na watu weusi nchini marekani ambayo
Ellijah hakutaka yaongelewe wala kupambaniwa.
Pia,
kwa nguvu ya Malcom, viongozi wa jumuiya ya kiislam walimwona ni kama
ana wapiku (kama hujui Kiswahili hapa umekwisha) namaanisha kuwazidi.
Kila sehemu alikua anaonekana Malcom na walimtuhumu anataka kutumuia
jumuia ya waislam kwa maslahi yake binafsi (eti kujipatia nguvu kama
mpambanaji) nimeamini kuna watu ni waswahili hata wazaliwe ulaya.
Kubwa zaidi ni pale Malcom X alipoongea kuhusu kifo cha John Kennedy,
Ellijah alikataza mtu yeyote kwenye NOI kuongea kuhusu kifo cha John
Kennedy. Wakati wa mahojiano na waandishi wa habari, Malcom alishindwa
kuvumilia akajibu
Wakati nikiwa mfugaji wa kuku nyumbani kwetu, nilikua sishangai pale kuku wanaporudi zizini kulala “the chickens coming home to roost.”
Yani watazurula weee ila lazma warudi tu nyumbani. Kifo cha Kennedy ni
sehemu tu ya ukatili wanaofanyiwa watu weusi, waislam na nchi maskini au
wale wote wasio kwenda sawa na falsafa za marekani, kwamfano Russia na
Cuba. Sasa wanarudiana wenyewe kwa wenyewe. Kifo cha Kennedy ni sawa na
kuvuna kile unachokipanda “you reap what you sow”. Hii speech ilivuruga ulimwengu, alipewa suspension ya siku 90 na ELLIJAH MOAHMED na ndio ikawa MAZIMA, hakurudi tena . Wengi walimwona kama msaliti wa shirika, na alipokea vitisho vingi vya kifo kutoka ndani ya kundi.
Malcolm akaamua kuanzisha mashirika mawili mapya, Muslim Mosque, Inc (MMI) na the Organization of Afro-American Unity (OAAU). Kama
ilivyokuwa kwa mashirika mengi ya haki za raia na wanaharakati, Malcolm
alikuwa akifuatiliwa karibu na serikali , Wakiwemo FBI chini ya babu
yangu EDGER HOOVER. Kweli snitch yupo kila sehem, yani hadi ndani ya
misikiti kuna mtu anatumika kutoa siri za kiongozi?, tena hasa simu zake
zilikua zinarekodiwa. Kwenye movie Fulani inayoitwa Godfather of Harlem , Malcom walipomwambia kuhusu kufuatiliwa kwake na jumuiya ya waislam pamoja na FBI alijibu “sina cha kuficha, waache wanifuatilie”
"walimwona
kama tishio," "Walifanya kazi ya kudhoofisha juhudi zake, kuunda na
kuzidisha mzozo na kumjengea maadui ili kumsababishia hata kifo chake."
Hapa MALCOM anawindwa na serikali na anawindwa na umoja wa waislam chini
ya Ellijah Moahmed, kumbuka alishapokea vitisho mara kadhaa.
Wiki
moja tu kabla ya kuuawa kwake, nyumba ya Malcolm X katika Jiji la New
York iliwashwa moto wakati yeye, mkewe Betty Shabaz na watoto wao wanne
walikuwa wamelala ndani. Hakuna mtu aliyewahi kushtakiwa kuhusiana na
tukio hilo. Ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa, ikawa ni dhahiri kwa
Malcolm na wale walio karibu naye kwamba alikuwa katika hatari kubwa.
Siku ambayo Malcom aliuawa.
Kwenye
mkutano wake kulikua na watu zaidi ya 400, na hakukua na ulinzi wowote
wa askari.. jambo ambalo halikua la kawaida. Kumbuka Malcom alirithi
tabia ya kutokusachi watu toka akiwa NOI hivyo wengi waliingia bila
kizuizi. Baada tu ya kusimama stejini alipigwa risasi Nyingi sana, siwez
kusema idadi kwamaana kila mtu anataja idadi yake, nimewahi kuona sehem
wanasema alipigwa risasi 21.
Talmadge Hayer
alipigwa risasi ya mguu na walinzi na kukamatwa wakati anajaribu
kutoroka kabla ya polisi kufika. Butler na Johnson, walikamatwa wiki
moja baadaye baada ya kushukiwa pia kuhusika na tukio hilo. Butler na Johnson walikuwa wanachama mashuhuri wa Harlem NOI.
New York City Police Department
(NYPD) Waliripoti kifo cha Malcom kwa kusema "jumuiya ya waislam
imemuua Malcom X “ "Walidhani ni mauwaji yaliyotokea kwasababu ya
upinzani kati yao."
Mahakamani sasa, Hayer alikiri kuwa sehemu ya mpango wa kumuua Malcolm, lakini akashuhudia kwamba Johnson na Butler hawakuhusika, walireport New York Times Machi 1, 1966. Wakati wa kesi hiyo, Hayer hakutaja mtuhumiwa mwingine yeyote.
Hakukuwa
na ushahidi wa kumuunganisha Butler au Johnson na uhalifu huo. Butler
alijitetea kuwa, siku ya kifo cha Malcom alikuwa zake nyumbani anauguza
kidonda cha mguuni na daktari wake alisimama kizimbani kumtetea mgonjwa
wake. Hakuna wa kuficha ukweli bwana, mwisho wanaume wote watatu
walipatikana na hatia mnamo 1966 nahukumiwa kifungo cha maisha jela.
Liz
Mazucci, Mtafiti Mkuu wa wa historia ya Malcolm X anasema, tukio lile
la kinyama halikuchunguzwa kwa umakini na polisi, walifanya kana kwamba
ni ripoti ya mchezo wa dance wakati ni mauwaji ya mtu mashuhuri na
tegemezi kwa wamarekani
Mnamo
1977 na 1978, Hayer aliwasilisha hati mbili zinazo endelea kusema
kwamba Butler na Johnson hawakuhusika katika mauaji hayo. Hata hivyo,
Hayer aliwataja wanaume wanne - wote walitoka NOI. Alidai kwa pamoja
walipanga mauaji ya Malcolm X mnamo Mei 1964. Alisema alifuatwa na watu
wawili kati ya wanne ambao walimwambia kwamba Malcolm X anapaswa kuuawa .
Baadaye walikutana na wanaume hao wengine wawili na kujadili jinsi
watakavyotenda uhalifu huo.
"Nilikuwa na upendo na Heshima kubwa kwa Elija Moahmed," kwa heshima yake niliona hili jambo lazima nilitimize.
Siku tano baada ya kuuawa, Muhammad alikataa kuhusika na mauaji hayo, na kusema "Malcolm X alikipata kile alichokihubiri."
Utekelezaji wa sheria haukufuatilia uchunguzi wowote kwa wanaume hao na kesi hiyo haijafunguliwa tena.
Butler alitolewa mnamo 1985. Johnson aliachiliwa mnamo 1989 na akafa mnamo 2009. Hayer aliachiliwa mnamo 2010.
Kwa miaka mingi, Betty Shabaz (Mke wa Malcom X) na familia yake walituhumu Jumuiya ya Uislam na kiongozi wake, Louis Farrakhan,
juu ya kupanga mauaji ya mumewe. Kumbuka Luis ni moja kati ya vijana
ambao walifundishwa kazi na Malcom X. Na baadae kuitwa Luis X Kama
alivyoitwa Malcom. Malcom alipojiondoa (NOI) Alimwacha Luis AKIWA KIJANA
CHIPKIZI. Luis aliwahi kuandika waraka magazetini kuwa Malcom Amemkosea
Elijah na wanachama wengine hivyo muda wote anamwombea afe tu. Luis
Farrakhan.
Mnamo 1995, binti ya Shabaz Qubilah
alishtakiwa kwa kuajiri muuaji kumuua Farrakhan. Farrakhan alimtetea
Qubilah na kujitetea kuwa hakuwahi kupanga wala kusababisha kifo cha
baba yake.
0 Comments