ACHANA NA BLACK PANTHER WALE PAKA Au movie ya Wakanda
Leo
nakupa historia/ machache kuhusu chama cha Black Panthers.... walioishi
kwa falsafa za Malcom X na kusambaratishwa kwa Hila za FBI
Kama unaikumbuka historia ya tupac na Mama yake Afeni Shakur
Afeni
alikua mwanajumuia wa Black Panther, harakati zilimuonjesha jela... na
hata ujauzito wa Tupac ni alamanusra ajifungue gerezani... lakini
alitolewa na kujifungua nje
Mwaka 1969 Pete O'Neal alikamatwa
kwa kosa la kusafirisha silaha (Bunduki) ndani ya mipaka ya marekani na
mwaka 1970 alipatwa na hatia na kuhukumiwa miaka 4 jela, lakini aliwahi
kufanikiwa kutoroka yeye pamoja na mke wake Charlotte O’Neal na kufanikiwa kufika nchini Algeria na baadae Tanzania ambapo walipokelewa vizuri na raisi wa wakati huo Julius Nyerere ambaye alikua muumini mkubwa wa ujamaa (Black Panthers walikua wajamaa pia) na kupatiwa makazi mapya Tanzania ambapo wanaishi hadi leo hii.
Geronimo Pratt ambaye
alikua kamanda wa cheo cha juu kabisa ndani ya black panther na baba
mlezi wa mwanamuziki Tupac Shakur, alihukumiwa miaka 27 jela na kutoka
mwaka 1997. Baada ya kutoka aliishtaki serikali kwa kumfunga kimakosa na
kulipwa fidia yake. Baadae aliamua kuja kuishi Tanzania na kufariki
Arusha June 2, 2011
Tuikumbuke mistari hii miwili “FID q, Professional “ Mwanaharakati kama Geronimo Pratt I am a professional
Ibra Da Hustler kwenye mchizi wangu RIMIX anamtaja pia, sina hakika kama napatia mistari ila nahisi kama alisema bila kumsahau the one and only Geronimo Pratt remember when we sat, what we talked about ilikua fact
FAHAMU MACHACHE KUHUSU BLACK PANTHERS
The
Black Panthers, pia walijulikana kama chama cha Black Panther, shirika
la kisiasa ambalo lilianzishwa mnamo 1966 na vijana: Huey Newton na
Bobby Seale wakiwa na dhumuni la kupinga ukatili wa polisi dhidi ya
jamii ya watu wenye asili ya Kiafrika . Msukumo mkubwa waliupata baada
ya kifo cha Malcom X , wengi hudhani Malcom alikua ndiye muasisi na
kiongozi wa kikundi hiki. Ila ukweli ni kwamba aliwaongoza kiimani na
falsafa tu. Wakitambulishwa kwa mavazi yao meusi na mitindo ya kofia
nyeusi (berets ) Panthers walipanga doria zao wakiwa na silaha kwenye
maeneo kama Oakland na miji mingine ya Marekani. 1968 hapa kikundi ndipo
kilipoanza kuwa cha moto kikiwa na wafuasi wapatao 2000. Shirika
lilikosa watu wengi hapo baadae kwasababu ya mivutano ya wenyewe kwa
wenyewe, vifo kwenye mashambulizi mbalimbali na shughuli za ujasusi za
FBI ambazo zililenga kudhoofisha chama hiko.
Waanzilishi wa Chama cha Black Panther , Huey Newton na Bobby Seale walikutana mnamo 1961 wote wawili wakiwa wanapinga sherehe iliuofanyika chuoni ya Pioneer Day
siku ambayo ililenga kuwakumbuka watu wa kwanza kufika kwenye mji huo
(mwaka 1800) na kusahau kuwapatia heshima watu weusi ambao pia
walitangulia kufika kwenye mji huo wa Magharibi
Seale na Newton waliunda Kikundi cha kuelimisha watu kuhusu ukweli wa historia ya watu weusi chuoni hapo.
Walianzisha
Black Panthers baada ya kuuawa kwa Malcolm X kama nilivyoelezea hapo
juu na baada ya polisi huko San Francisco kumpiga risasi kijana mweusi
asiye na silaha Matthew Johnson.Na ndio sababu ya
shughuli ya mwanzo kwa panthers ilikua ni kujilinda na kusimamia
mienendo na shughuli za polisi huko Oakland na miji mingine.
Walipoanzisha
programu kadhaa za kijamii na kujihusisha na shughuli za kisiasa,
umaarufu wao ulikua unakua. Panthers walipata misaada kutoka kwa watu na
vikundi kadhaa vinavyojishughulisha namasuala ya kijamii huko Los
Angeles, Chicago, New York na Philadelphia.
Shughuli za Kisiasa na Mipango ya Jamii
Newton
na Seale walikijenga kikundi/chama kwa itikadi ya ki Marxist (KIJAMAA).
Walielezea maoni yao kifalsafa na malengo ya chama chao kisiasa katika
mfumo waliouita TEN POINT PROGRAM
Programu ya Pointi Kumi ilijumuisha sehemu mbili: Ya kwanza, WHAT WE WANT (TUNACHOHITAJI)Walieleza Chama cha BlackPanther kinataka nini kwa uongozi wa kibaguzi wa marekani wakati huo, na upande wa pili wa TUNACHOAMINI ( WHAT WE BELIEVE) hapa wanaelezea maoni ya kifalsafa ya chama hicho na haki ambayo Wamarekani Weusi wanapaswa kuwa nayo,Kwa mfano
,
sehemu moja inasema kwamba, "Tunaamini kuwa serikali hii ya ubaguzi wa
rangi imetuibia sana na sasa tunataka watulipe deni letu la hekari
arobaini na punda wa kulimia (Forty acres and a mule).
Hekari
40 na punda viliahidiwa miaka 100 iliyopita kama malipo ya kazi ya
watumwa na mauaji ya watu weusi ". Inaendelea kusema kuwa "Tutakubali
malipo haya kwa mtindo wa fedha ambayo itasambazwa kwa watu wa jamii
zetu ." Newton na Seale waliamini kwamba jamii ya watu weusi ilikuwa
imenyimwa faida hizi kwa miaka, na kwamba njia pekee ya kusahihisha
ukosefu huo wa haki ilikuwa katika ulipaji wa mali ambazo walipoteza kwa
miaka mingi ya utumwa.
Wakati
wa Panthers , serikali iliwatazama kama genge la wahalifu wakati wao
binafsi wakijiona kama chama cha kisiasa ambacho lengo lake lilikuwa
kuwafanya Wamarekani zaidi wenye asili ya Kiafrika wateuliwe kwenye
nyadhifa za kisiasa. Hawakufanikiwa kufika huko. Mapema miaka ya 1970,
juhudi za ujasusi wa FBI, shughuli za uhalifu na ugomvi wa ndani baina
ya wanachama wa kikundi ulidhoofisha chama na nguvu ya kisiasa.
Tukumbuke
walijaliwa pia kuanzisha miradi kadhaa ya kijamii kama programu za bure
za kuwapatia chakula watoto wa shule na huduma za bure za afya kwa
jamii 13 za wamarekani weusi ndani ya nchi ya marekani.
MIKANGANYIKO NA VURUGU NDANI YA BLACK PANTHER
Panthers
walihusika katika vurugu nyingi na polisi. Mnamo mwaka wa 1967,
mwanzilishi/muasisi, Huey Newton alidaiwa kumuua afisa wa polisi wa
Oakland John Frey. Newton alihukumiwa kwa mauaji mnamo 1968 kifungo cha
miaka 2 hadi 15 (kwa miezi 22 alikaa lockup na aliruhusiwa kuonana na
watu 10 pekeake kwa muda wote huo). Eldridge Cleaver, mhariri wa gazeti
la Black Panther, na mwanachama wa miaka 17 wa Black Panther, Bobby
Hutton, walihusika katika majibizano ya risasi na polisi mnamo 1968
ambapo Hutton alifariki na maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa.
Migogoro
ndani ya chama mara nyingi ilibadilika kuwa vurugu pia. Mnamo mwaka
1969, Mwanachama wa Black Panther, Alex Rackley aliteswa na kuuawa na
watu wengine weusi wa Panthers ambao walimhisi kuwa ni chawa wa polisi (anavujisha taarifa zao).
Mtunza barua na vitabu wa Black Panther Betty Van Patter
alipatikana akiwa amepigwa na kuuawa mnamo 1974. Hakuna mtu
aliyeshtakiwa kwa kifo hicho, ingawa wengi waliamini kuwa uongozi wa
chama uliwajibika.
FBI NA COINTELPRO (COunter INTELligence PROgram)
Huu ni mkakati wa FBI wakati huo, kuhakikisha vyama na wanaharakati wote wanakatwa mikia
Ujumbe wa ujamaa wa Black Panther nautofauti wa kimtazamo wa kitaifa uliwafanya kuwa shabaha ya mpango wa siri wa FBI uitwao COINTELPRO.
Mnamo
1969, FBI ilitangaza Black Panthers kuwa ni shirika la kikomunisti na
adui wa serikali ya Marekani. Mkurugenzi wa kwanza wa FBI, J. Edgar
Hoover, mnamo 1968 alisema The Black Panthers, "Moja ya vitisho vikali
kwa usalama wa taifa."
FBI ilifanya kazi ya kudhoofisha Panthers
kwa kutumia ubishani uliopo kati ya wenyewe kwa wenyewe. Pia Walifanya
kazi ya kudhoofisha na kuondoa mpango wa chakula bure mashuleni kwa
watoto (mpango ulioanzishwa na Panthers) na programu zingine za kijamii.
Mnamo
mwaka wa 1969, polisi wa Chicago waliwashambulia kwa bunduki na kuwaua
wanachama wa Chama cha Black Panther Fred Hampton na Mark Clark, ambao
walikuwa wamelala ndani ya nyumba yao.
Walisema
zilipigwa risasi zaidi ya miamoja na kuwa mapambano makali kuwahi
kutokea ila ukweli ni kwamba uchunguzi ulibaini upande wa Panther
walirusha risasi moja tu kwa polisi.
Chama cha Black Panther kilifutwa rasmi mnamo 1982.
Lakini chama kipya cha Panther kiliundwa huko TEXAZ mwaka 1989.
Washiriki wa Chama cha Asili cha Black Panthers walisema hakuna
uhusiano kati ya Chama kipya cha Panther na Panthers asilia.
0 Comments