ELIMU BORA KWA WOTE TANZANIA INAWEZEKANA
Ninandoto ya kuhakikisha watoto wetu wote nchi nzima wanapatiwa elimu bora inayojitosheleza, isiyowabagua kutokana na kipato cha wazazi wao, itakayowapa taaluma na nidhamu, hekima na maarifa, itakayowawezesha kuajiriwa na kujiajiri, itakayowawezesha kuthubutu na kuwajengea uadilifu.
Licha ya mafanikio makubwa yaliopatikana katika elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu katika awamu ya nne ambayo ni ongezeko la shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu, uboreshaji wa miundombinu ya elimu, ongezeko la udahiri wa anafunzi katika ngazi zote, ubora wa elimu chini umeendelea kushuka mwaka hadi mwaka.
Licha ya sababu mbalimbali zilizotolewa kuchangia kuporomoka kwa ubora wa elimu nchini; Sababu kuu ni uwepo wa Soko huria katika sekta ya elimu, Elimu kwa sasa ni BIASHARA HURIA. Hali ilivyo sasa ubora au udhaifu wa elimu wanayopatiwa watoto wetu ni kutokana na kipato cha wazazi wao.
Watoto wa Matajiri wanapatiwa elimu bora katika shule bora za binafsi lakini watoto wa wenye kipato cha kati na masikini wanapatiwa elimu dhaifu katika shule za Serikali au shule binafsi ambazo ubora wa elimu hautofautiani na ule wa shule za Serikali. Watoto wa masikini wanasoma kwenye shule za Serikali ambazo hazina walimu wa kutosha, walimu waliopo sio wabobezi katika masomo waayofudisha. Shule hazina vitendea kazi vya kutosha kama vile vitabu, mbao za kufundishia zimechakaa, hakuna maabara, mazingira mabovu ya kufundishia na kujifunzia, afya za watoto wetu zimewekwa rehani kwa maana hakuna matundu ya vyoo ya kutosha. Hata hivyo vyoo vyenyewe ni vichafu, walimu wamepoteza morali ya kufundisha kutokana na ujira mdogo na mazingira ya kufundishia yasiowaridhisha yanayochochea malalamiko na migomo isiyoisha.Watoto wa wanyonge ndio wanaopatiwa elimu dhaifu, kwa sababu vipato vya wazazi wao ni vidogo na hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule za watu binafsi.
Watoto wa wenye nacho yaani Watanzania wanaofanya kazi katika ofisi nyeti za Serikali na wafanyabiashara wanasoma katika shule Binafsi (Private schools) zinazojulikana kama International and English Academy Schools na wengine wanapelekwa kusoma nje ya nchi ili kupatiwa elimu bora. Watoto hawa wanapatiwa elimu bora kwa sababu kila kilicho kikwazo cha elimu bora katika shule za Serikali hakipo kwenye shule hizi binafsi. Shule binafsi zina walimu wabobezi wa kutosha, wanaolipwa ujira unaokidhi matakwa yao, mazingira ya kufundishia na kujifunzia ni mazuri, vifaa vya kujifunzia kama vile vitabu, computa, maabara, madaftari vipo vya kutosha. waafunzi wanapatiwa chakura bora asubuhi na mchana, watoto wanafundishwa vizuri kwa maneno na vitendo. Hawapati usumbufu wowote kwani hawafagii pia hupelekwa shule na kuludishwa yumbani kwa mabasi maalumu.
Kwa maaa hiyo mazingira ya upatikaaji wa elimu nchini Tanzania hayapo Fair, PESA ZA WAZAZI ndio mwamuzi(Determinant) wa ubora au udhaifu wa elimu anayopatiwa mtoto.
Vyuo vikuu navyo VIMEPOTOKA, ubora wao umebaki kweye Vision na Mission. Wanachokifanya kwa sasa ni Kudahiri wanafunzi wengi ili wapate pesa. Kila kukicha wanaongeza Kozi(program mpya) ili kupata wanafuzi wengi. Wamesahau kabisa ya kwamba wajibu wao ni kuzalisha Watalaamu na sio kulundika wanafunzi madarasani.
Mambo ya kujiuliza
• Kama shule za Serikali zikitoa elimu bora, nani atatamani kumpeleka mwanae katika shule za watu binafsi ambazo ada zake ni za juu sana?
• Shule za Serikali zinawezaje kutoa elimu bora ikiwa shule za watu binafsi zipo? Kumbuka ya kwamba kufanya hivyo ni kuhatarisha soko la watu binafsi.Watu binafsi lazima waendelee kuhujumu utoaji wa elimu katika shule za Serikali ili shule zao zipate wanafunzi.
• Viongozi wanawezaje kuboresha shule za Serikali wakati watoto wao HAWASOMI HUKO?
• Shule za Serikali lazima ziendelee kutoa elimu dhaifu ili Shule za watu binafsi zipate wanafunzi.
Mapedekezo
Watanzania wote ni sawa na kila mtu anastahili elimu bora na kuthaminiwa utu wake. Ili kuhakikisha Serikali inatoa elimu bora kwa wote lazima watoto wa masikini na matajiri wasome katika shule za Serikali. Ikiwa tutafanikiwa kwa hilo viongozi wa Serikali na wafanyabiashara watatoa jitihada za kutosha katika kupambana na changamoto au vikwazo vya upatikanaji wa elimu bora katika shule za Serikali nchini na kwa pamoja tutaweza kuboresha elimu kama Taifa. Lazima tuishauri na ikilazimika kuishinikiza Serikali kuondoa MATABAKA kwenye elimu. Uwepo wa Matabaka katika utoaji wa elimu ndio kitovu cha kushuka kwa ubora wa elimu mwaka hadi mwaka hususan katika shule za Serikali.
Vyuo vikuu vidhibitiwe, lakini yote yamesababishwa na Elimu kuwa BIASHARA
0 Comments