Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ atakiwa kuchunguzwa baada ya kuonyesha kidole cha kati bungeni

June 10 2016 Naibu spika  Dk Tulia Ackson alitangaza bungeni kuiagiza kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge kufanya uchunguzi wa kitendi cha Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ’Sugu’ kudaiwa kuonyesha ‘dole’ bungeni kitendo kinachoashiria matusi.

Akisoma mwongozo Naibu spika Tulia amesema…>>>’kitendo hicho kilifanyika wakati Joseph Mbilinyi alipokuwa akitoka ukumbini baada ya kuwasilisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni ‘

‘Jambo linaloombewa mwongozo linahusu maadili ya bunge, mwongozo huo unatokana kitendo cha mbunge kuonyesha kitendo chenye tafsiri ya matusi ‘

‘Kutokana na maelezo ya hapo juu na masharti ya kanuni, naelekeza kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge ifanye uchunguzi kuhusu kitendo kinachodaiwa kufanywa na mheshimiwa Joseph Mbilinyi na kuchukua hatua stahiki‘

Post a Comment

0 Comments