Saikolojia ya mkakati wa Copper

SAIKOLOJIA YA MKAKATI WA COOPER
Baada ya miaka mingi ya upelelezi na kujiuliza
maswali mengi hatimae mwaka 2007 FBI walitangaza
kwa umma baadhi ya mambo waliyoyabaini katika
mkasa mzima wa D.B Cooper.
Kwa mfano siku ya tukio Cooper alihitaji parashuti
moja tu ili aweze kuruka lakini aliwaagiza kuwa
anahitaji maparashuti manne. FBI wanaamini kuwa
Cooper alitoa maagizo ya dizaini hii ili kupandikiza
wazo kwa vichwani mwa maofisa wa FBI kuwa
kulikuwa na uwezekano akaruka na mateka ambao
watatumia maparashuti mengine matatu yaliyobaki.
Hii iliwalazimu FBI kumpatia maparashuti manne
ambayo hayana hitilafu au ubovu wowote. Na
iliwachukua muda sana kubaini kuwa Cooper alicheza
na akili zao bila wao kujua.
Pia uchaguzi wa kuiteka Northwest Orient Flight
305 haukuwa wa bahati mbaya. FBI wanaamini kuwa
Cooper alifanya uchunguzi wa kina na kuchagua
kuiteka ndege hiyo. Kumbuka kuwa Orient Flight
305 ilikuwa ni aina ya ndege ya Boeing 727.
Kwa kipindi hicho Boeing 727 ndio zilikuwa ndege
pekee ambazo zilikuwa na uwezo wa kufunguliwa
mlango wa nyuma mkiani ikiwa bado iko angani. Kitu
hiki kilikuwa hakijulikani kwa raia na hata watu wa
ndege wenyewe walikuwa hawafahamu jambo hili. Na
taarifa hii ilifichwa kwasababu kwa kipindi hiki
haikuwa kitu cha kawaida kwa ndege ya abiria kuwa
na ubunifu wa aina hii.
Watu pekee ambao walikuwa wanafahamu suala hili
na kuwahi kutumia advantage ya ubunifu huu
walikuwa ni CIA ambao walitumia ndege kama hii
kudondosha mizigo na maafisa wao katika maeneo
husika katika vita ya Vietnam.
Pia injini za Boeing 727 zilikuwa juu kidogo tofauti
na ndege nyingine za abiria ambazo injini zake
zilikuwa chini chini karibia usawa wa madirisha.
Kumbuka kuwa injini ya ndege ikiwashwa ikiwa
inazunguka kitu chochote kikipita mbele yake
kinavutwa na kumezwa kwenye injini na kuharibiwa
au injini yenyewe kupata hitilafu. Hivyo basi
uchaguzi wa kuruka kutoka kwenye Boeing 727
ilimaanisha kuwa ilipunguza hatari ya mrukaji
kuvutwa na kumezwa na injini.
Pia FBI wanaamini kuwa Cooper alifahamu kuwa
Boeing 727 ilikuwa na teknolojia mpya ambayo
iliruhusu kujaza mafuta kwenye matanki matatu ya
ndege kwa kutumia tundu moja tu. Kama isingekuwa
na teknolojia hiyo hiyo ya kujaza mafuta kwa tundu
moja tu FBI wangeweza kutumia mwanya wa gari la
kujazia mafuta likiwa linazunguka upande mwingine
wa ndege kupenyeza maafisa wao.
Pia Boeing 727 ilitoa advantage nyingine katika
ufunguaji wa mlango wa nyuma wa ya mkia wa
ndege ambapo ukiwasha tu kifaa cha kufungua
mlango huo hata rubani aliye mbele hawezi
kuufunga. FBI wanaamini Cooper alilifahamu hili
ndio maana baada ya kuwafungia watu aliobaki nao
kwenye chumba cha rubani. Alifungua mlango wa
nyuma kwa kujiamini na kuruka.
Pia Boeing 727 ilikuwa na ubunifu mwingine adhimu
tofauti na ndege nyingine kwa kuwa ilikuwa unaweza
kucontrol speed na mwinuko wa ndege 'manually'
hata ukiwa katika sehemu ya kukaa abiria, pia kwa
kipindi hicho Boeing 727 ndio ilikuwa ndege pekee
ya abiria ambayo ilikuwa na uwezo wa kugeuza
mabawa yake ili yakae katika nyuzi 15.
FBI wanaamini kuwa Cooper alifanya utafiti wa kina
na kuweka mkakati kabambe kabla ya kutekeleza
tukio na alitumia advantage zote hizi za ndege ya
Boeing 727 ili kutekeleza tukio lake kwa ukamilifu
wa 100%.
Lakini jambo lingine la muhimu zaidi ilikuwa ni
uchaguzi wa siku ya tukio. November 24.
Kwanini?? Baada ya tukio FBI kugundua Cooper
alikuwa ameruka nyikani wazo mojawapo ambalo
walilipata ni kwambHa kwakuwa sehemu aliyoruka
ilikuwa mbali mno na makazi ya watu, hivyo basi
ingemchukua Cooper takribani siku hata tatu
kusafriri ili kurudi mtaani. Kwahiyo FBI walidhani
kwa kuwa Cooper asingeliwezakutumia siku moja
kusafiri kurudi mtaani hivyo basi kama kesho yake
wangembelea kila ofisi na maeneo ya kazi kukusanya
orodha ya watu ambao hawajatokea kazini lazima
watu hao mmoja wao angekuwa ni Cooper.
Lakini hii ilikuwa haiwezekani! Kwanini? Kwasababu
November 24 usiku wake ulikuwa ni sikukuu ya
'Thanks giving' maana yake ni kwamba kesho yake
haikuwa siku ya kazi. Mbaya zaidi November 24,
1971 ilikuwa ni siku ya Jumatano kwahiyo kesho
yake alhamisi pamoja na ijumaa zilikuwa siku za
sikuu na siku zilizofuata zilikuwa ni weekend.
Kwahiyo hii ilimpa Cooper siku nne za kutosha kabisa
kusafiri kutoka nyikani mpaka mtaani. Na kama
alikuwa mfanyakazi ofisi fulani maana yake
Jumatatu aliingia ofisini kama watu wengine.!!! FBI
wakapiga saluti..!

Post a Comment

0 Comments