Kwa kuitazama vyema historia ya Marekani, utagundua kuwa Marais wote wa nchi hiyo waliochaguliwa katika miaka inayoishia na 0, ukiondoa mwaka 1840, ama waliuawa au walikufa wakiwa madarakani kutokana na kile kilichoonekana kuwa ni kifo cha kawaida.
Mwaka 1840 Marekani ilikuwa na Rais wa nane, Martin Van Buren, aliyetawala kuanzia 1837-1841. Kinachotia shauku zaidi ni kwamba matukio hayo hutokea, au tuseme yalikuwa yakitukia, kila baada ya miaka 20 kwa miongo mingi iliyopita.
Robert Ripley aliyekuwa mchoraji maarufu wa katuni na mtunzi wa kitabu cha vichekesho chenye jina Ripley's Believe It or Not katika jalada lake, aliwahi kutaja mtindo wa kila miaka 20 ya vifo vya Marais wa Marekani kati ya mwaka 1840 na 1920 kisha, katika sentensi moja iliyo chini ya katuni moja, akaandika “…1940!?”
Aliweka alama ya ulizo kwa kuwa hakujua kile ambacho kingetokea mwaka 1940 kwa sababu kilichapishwa mwaka 1935, miaka mitano kabla ya mwaka aliouwekea alama ya ulizo (?).
Ripley alikuwa akifikisha ujumbe kamili kwa wasomaji wake, lakini kwa kuwa wengi walimchukulia kama mchekeshaji tu, walipuuza, lakini alijua yaliyokuwa yakitendeka. Alikuwa akipitisha ujumbe wake kwa njia ya vichekesho, na watu hawakuupokea.
“…1940!?” ilidokeza kwamba Rais wa Marekani aliyechaguliwa mwaka huo angekufa angali akiwa Rais wa nchi. Je, Ripley alikuwa akichekesha tu? Lilikuwa jambo la bahati mbaya au kujirudia kwa historia hata Ripley akajua kwa hakika kile ambacho kingetukia? Rais huyo hakufa akiwa madarakani? Haya ni maswali ya kitoto?
Tangu alipokuja duniani Jumatatu ya Januari 30, 1882, kupitia kwa baba na mama yake, James Roosevelt na Sara Delano Roosevelt, Franklin Delano Roosevelt hakujua kuwa Jumanne ya Aprili 4, 1933 ndipo angekuwa Rais wa 32 wa Marekani. Na hata baada ya kujua hivyo, hakujua kuwa kuna mengine ambayo hakuyajua.
Wamarekani walimchagua tena mwaka 1936 dhidi ya mpinzani wake, Alfred M. Landon. Tofauti na marais wengi wa nchi hiyo, Roosevelt alitumikia zaidi ya vipindi vitatu. Lakini hilo si muhimu kwa maana ya Robert Ripley.
Alipochaguliwa kwa kipindi cha tatu mwaka 1940 dhidi ya Wendell Willkie, akatimiza kile kilichotazamiwa. Ikajulikana kwa watu wachache sana wa ulimwengu huu waliojua siri kuwa angekufa akiwa madarakani.
Hata hivyo alisonga mbele. Ukaja uchaguzi mwingine mwaka 1944, Roosevelt akamshinda Thomas E. Dewey. Lakini hilo halikuondoa ukweli kuwa alichaguliwa mwaka 1940. Alhamisi ya Aprili 12, 1945, Roosevelt, akiwa katika kipindi cha nne cha kutawala kwake, akafa angali akiwa Rais.
Hiyo ni bahati mbaya? Au ni kujirudia kwa historia? Kama twafikiri hivyo, tuwe makini zaidi. Mwanzoni mwa karne ya 20 mwanamke mmoja wa Australia aliyeitwa Foster Turner, akiwasiliana kwa njia ya ‘upepo’ na mtu aliyeitwa Arthur Conan Doyle, walitabiri kuzuka kwa Vita Kuu I na matokeo yake. Vyote alivyotabiri vikatokea. Je, alitabiri au alijua mipango iliyokuwapo? (Soma kitabu cha Max Freedom Long kiitwacho The Secret Science Behind Miracles).
Kitabu kiitwacho How to Succeed cha Brian Adams © 2004 (uk. 5) kinasema hivi katika aya ya pili: “Mauaji ya John F. Kennedy yalitabiriwa na mbashiri anayejulikana zaidi Marekani (mwanamke ambaye hakutajwa jina). Alitaja kwa usahihi kabisa wakati, mahali na tarehe ambayo mauaji hayo yangefanyika. Kwa bahati mbaya, onyo lake halikusikilizwa.”
Huo tutauita utabiri? Huyu ni Rais aliyechaguliwa mwaka 1960, mwaka unaoishia na ‘0’, na huyo aliyetabiri ni Mmarekani. Tunajuaje kama huyo ambaye mwandishi Brian Adams anamwita mbashiri alijua mipango ya kuwaua watu hawa hata akajua wakati, tarehe na mahali ambapo mauaji ya Kennedy yangefanyika?
Mwanamke huyo mbashiri ambaye kitabu hicho hakikumtaja jina, siye peke yake ‘aliyetabiri’ kuuawa kwa Kennedy. Mbona Robert Ripley mwaka 1935 alitabiri kifo cha Roosevelt miaka kumi baadaye ambaye pia alifariki akiwa madarakani? Je, hakuuawa? Au tuseme hakuuawa kwa njia ile ile aliyouawa John Kennedy au Abraham Lincoln?
Kwa kutazama vile vipindi vya kila miaka 20, wanajimu wengi, au wale waliojiita wanajimu, walibashiri kifo cha Rais John Kennedy mara alipochaguliwa kuwa Rais mwaka 1960. kikatokea hatimaye.
Kwa njia hiyo hiyo ilitazamiwa pia kwamba hata Rais Ronald Wilson Reagan angeuawa au kufa ‘kifo cha kawaida’ angali Rais, jambo ambalo lilikaribia kabisa kutimia.
Jumatatu ya Machi 30, 1981, akiwa na umri wa miaka 70 na baada ya kukaa ofisini kwa siku 69 tu tangu aapishwe, Rais Reagan alijeruhiwa kwa risasi tano au sita zilizofyatuliwa na John Hinckley (25) na kukimbizwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu ya George Washington kufanyiwa upasuaji.
Kilichostua ni rais wa Marekani George W Bush ambae hakuuwawa hadi anatoka madarakani
Inasemekana kuwa sababu yeye na familia yote ya Bush tangu vizazi vingi vilivyopita wanajua na kushiriki mambo mengi huko Marekani. Hata George (Baba) Bush alijua, na pengine (aliandika mwandishi mmoja) alikuwa na mkono katika tukio la Reagan wakati yeye akiwa Makamu wake wa Rais.
Kwa kushangaza, marais waliochaguliwa katika miaka iliyoishia na ‘0’ wote walifariki wangali madarakani na walikufa katika miaka inayoishia na ‘1’, ‘3’ na ‘5’. Kwa hiyo, mwaka 2005 ulikuwa ndio wa George W. Bush. Lakini huo umepita.
Katika hili kuna mambo ya kutazama pia. Rais wa 12 wa Marekani, Zachary Taylor (1849-1850), alifariki dunia akiwa madarakani. Lakini hakuchaguliwa mwaka unaoishia ‘0’. Alichaguliwa mwaka 1848 na akafariki dunia mwaka 1850 kutokana na maumivu ya tumbo.
Ilisemwa kuwa ni kifo cha kawaida, lakini uchunguzi unaodokezwa na vielelezo vingi vya kihistoria ni kwamba bila kutambua Rais huyo alilishwa sumu iliyochanganywa na kemikali nyingi.
Haikuwa lazima Taylor achaguliwe mwaka ule wa ‘0’. Mwaka 1991, ikiwa ni miaka 141 tangu kifo chake, mwili wake ulifukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi upya kuthibitisha madai hayo.
Lakini, baada ya ‘uchunguzi’, serikali ya Marekani ilisema madai hayo ni ya uongo. Hakuna aliyetazamia serikali ingesema madai hayo ni ya kweli, kwani kwa kufanya hivyo ingekuwa serikali ndiyo iliyomuua Rais wao na hivyo kuharibu rekodi ya Marekani.
Tazama orodha ya marais hao ilivyo (miaka ya kuchaguliwa kwao ikiwa katika mabano). Thomas Jefferson (1800), alinusurika jaribio la mauaji dhidi yake, hatimaye alifariki dunia Julai 4, 1826. James Monroe (1820) naye alinusurika. Alifariki Julai 4, 1831.
William Henry Harrison (1840), alifariki akiwa Rais Aprili 4, 1841 kutokana na kichomi(?). Abraham Lincoln (1860), kama ilivyotajwa mara nyingi katika makala hii, aliuawa Ijumaa ya Aprili 15, 1865.
Wengine ni James A. Garfield (1880) aliuawa Julai 2, 1881. William McKinley (1900), aliuawa Septemba 19, 1901. Warren G. Harding (1920), aliuawa Agosti 2, 1923 kwa kulishwa sumu iliyowekwa katika chakula. Franklin D. Roosevelt (1940), alifariki Aprili 12, 1945 kutokana na kile kilichoitwa ‘kiharusi’, lakini kumbukumbu nyingi za matibabu yake hazijawahi kupatikana. John F. Kennedy (1960) aliuawa kwa risasi Novemba 22, 1963 na Ronald Reagan alikoswa koswa Machi 30, 1981, hata hivyo hatimaye akafariki dunia Juni 5, 2004.
Kuna marais wengine wa Marekani ambao waliwahi kunusurika. Lakini hii inaonekana kuwa ajali zaidi kuliko makusudi kama inavyoonekana kwa wengine waliotajwa hapo juu.
Sasa ndugu zangu hii ni bahati mbaya au ni kupangwa kwa haya matukio?
Kama yalipangwa ni nani aliyeyapanga?
0 Comments