Raia wa mshangano (songea) mkoani Ruruma,wagoma kumzika kijana aliyekijulikana kwa jina la Daniel Maundi (31) siku ya tarehe 20/2 aliyefariki siku ya tarehe 19/2 kwa ugonjwa wa jipu kwenye jino

Raia hao waliacha kaburi likiwa wazi na kulazimisha wazazi wazike pekeyao na kumlazimisha baba wa marehem akaonyeshe mahali alipomuweka mtoto wake baada ya yeye mwenyewe kukiri kwamba mtoto wake amemuweka maeneo ya magengeni na ule mwili utakaozikwa ni mgomba tu.Zoezi hilo lilisimamishwa na police kwa kuhofia kutokea kwa vurugu katika maeneo hayo 

Baadhi ya majirani wamesema kuwa,kijana huyo Daniel alikua na ugomvi wa mda na baba yake na siku chache kabla ya kifo chake walifikishana kwenye vyombo vya sheria kwa kile kinachodaiwa kwamba Danie alimshutumu baba yake kua ni mchawi 

Hata hivyo leo tarehe 21/02 kijana Daniel amezikwa kwenye makaburi ya mshangano bila uwepo wa baba yake mzazi katika eneo hilo.Danie ameacha watoto 5 na mjane mmoja

Tazama video wakati wa mazishi hayo
0 Comments