Huu ndio mkwanja atakaolipwa ‘Katy Perry’ kama Jaji wa American Idol

Ukiwa na kipaji raha sana!! Msanii wa muziki kutoka Marekani mrembo, Katy Perry ambaye wiki chache zilizopita alitangazwa na kituo Runinga cha ABC kuwa rasmi ndiyo atakuwa Jaji wa Shindano la American Idol, tayari wadau wa mambo wameshapata data za mkwanja atakaolipwa na waandaaji wa Shindano hilo.

Kate Perry

Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ, Kate Perry atalipwa kiasi cha Dola Milioni $25 sawa na Shilingi Bilioni 56 za Kitanzania, pesa ambayo ni ongezeko la Dola milioni $5 kutoka Dola milioni 20 ambazo alizipiga chini mwaka 2012 wakati waandaji wa American Idol walimuomba awe jaji mkuu wa tamasha hilo maarufu zaidi duniani.



Kwa mkwanja huo atakaolipwa Katy Perry atakuwa ndiyo msanii wa kwanza kulipwa mkwanja mrefu kama Jaji kwenye mashindano hayo maarufu duniani la kusaka vipaji vya kuimba ‘American Idol

Post a Comment

0 Comments