Kendrick Lamar asimamishwa na polisi,ajibu maswali bila kutumia umaarufu wake



Tofauti na mastaa wengine kabisa, Kendrick Lamar amesimamishwa na polisi wa Bev Hills weekend hii na kukubali kujibu maswali bila kutumia umaarufu wake ili polisi walegeze kidogo.
Polisi aliyesimamisha gari hio aliwasiliana na Kituo cha karibu cha polisi kuhusu leseni ya Kendrick Lamar sababu hakujua yeye ni nani na Kendrick hakutumia umaarufu wake kumaliza tatizo hilo.
Kendrick alisimamishwa barabarani akiwa na gari yake Nyeusi aina ya G-Wagon  na alionekana kuongea na askari huku kioo cha gari kikiwa kimeshushwa, haijulikani sababu ya kusimamishwa kwake.

Post a Comment

0 Comments