Utata akirudi

*Utata akirudi*

Na Humphrey Moris

Mwanamuziki Killah Priest (Walter Reed) wa kundi la muziki wa rap huko Marekani, panapo mwaka 1995 katika kibao chake alichokiita B.I.B.L.E (Basic Instructions Before Leaving Earth) ameimba;

    

    "I even learnt Caucasians were really the tribe of Edam,

    The white image of Christ, is really Cesare Borgia, and uhh,

    The second son of Pope Alexander, the Sixth of Rome,

    And once the picture was shown,

    That's how the devils tricked my dome…"

Tuachane na hayo

Wapo wengi wanaoamini katika kurudi kwake lakini uwepo wake tu unautata kwa wengi.
Wapo walioamini huyu jamaa alikua mweupe pee kwasababu ya sehemu aliyozaliwa
Na wapo walioamini ni mweusi tii kwasababu ya sehemu aliyokimbiziwa ili aungane na wenye rangi wenzake (ni rahisi sana kumtambua mtu wa rangi tofauti kati ya watu weeengi wenye rangi inayofanana labda ndio sababu ya kumpeleka kwa wenye rangi kama yeye)

*Akirudi*... tuombe awe wa rangi ile tunayoiona kwenye picture kwakua sisi wenye rangi hii ya *maandishi* ni wepesi sana kukubali tunayoambiwa na wao na kwa ushahidi wa hilo tunawaona wengi wetu wanaamini uwepo wa jamaa katika rangi ya picture na wachache katika rangi ya maandishi sasa sijui alifika kwaajili ya nani mtu huyu (ila atarudi)

Na kama atarudi kwa rangi hii ya maandishi basi watu wa rangi ile ya picture wooooote watamkataa na hawatomwamini na hii sio kwao tu bali hata sisi wenye rangi hii ya maandishi watampinga na kusema sio yeye waliyemdhania ... si unaijua rangi yetu bwana tunaamini sana linalosemwa na rangi ya picture ( *atapata waumini na wafuasi wachache sana* )

Na akirudi.... tutafurah akiweza kuzungumza lugha zote za wanaoamini katika yeye ila akizungumza lugha moja basi atakua alikuja kwaajili yao.Na wengine wote watamkataa japo watatokea watakaojifunza hiyo lugha ili kuwa nae pamoja (sina hakika na hili) ILA TUMSUBIRI ARUDI

Na Humphrey Moris

Post a Comment

0 Comments