Kama kuna moto mbona tayari tupo motoni

Wanasema baada ya haya maisha kuna upembuzi. kuna watakaopimwa na mzani wao kudondokea *peponi*  (naskia kuna raha sana huku) na wapo watakaodondokea *motoni* (simulizi zake humtisha hata muuwaji huku duniani).


Je mungu alituumba tuje kuishi kwa raha au shida? wakati huo unaambiwa *sio kua masikini ndio utauona ufalme wa mbingu* na wala sio kuwa tajiri basi ni wa motoni hapo siku ya mwisho. Wapo matajiri wanatenda mema sana na hivyo ufalme wa mbingu pia ni wao (hawa watakula raha mbinguni na duniani wanakula)
Wapo masikini na wataingia motoni kwakua hawana moyo safi (heri wenye moyo safi kwa maana watamwona mungu) kosa lao ni kutotimiza yampasayo kutoka kwa kile anachohitaji mungu.


*Masikini*
Maisha yake tu ya duniani ni moto tosha
*Serikali yake inamchoma
kazaliwa maskini anakufa maskini na sio kama alilala.. anataabika kupambana ila kama ilivyokawaida na kuna baadhi ya nchi kama India ukizaliwa koo maskini utakufa masikini au Kenya na Uganda.. uwe SLUM DWELLER alafu uje kuwa tajiri si rahisi japo inawezekana..kuzaliwa masikini na kuufikia utajiri sio kazi ndogo na wengi wanakufa wakiwa masikini au wakipata kidogo vinapotea na wanakufa maskini kwasababu (Poor people dont have time for investment, because poor pple are too busy try not to be poor) watu maskini hawana/hatuna muda wa kuwekeza kwakua tunapambana tusiwe maskini- haswaa kwenye mambo ya misosi, TULE TUISHI JAMANI


*Maisha yake yanamchoma
Pale masikini anapojitahid kuutafuta utajiri anatabika sana.
Wengi wamechomwa moto wakiwa wanautafuta utajiri hahaaa huyu akifa anakutana na moto mwingine huko juu kwaajili ya dhambi zake.


*Dini yake pia inamchoma
(anatia huruma sana masikin)
Baadhi ya dini huyu masikini akijaribu hata kuiba anakatwa mkono. Angezaliwa tajiri huyu sidhani kama angechomoa simu ya elfu 15 mfukoni mwa mtu


Hayo hayawez kumpata tajiri
*Tajiri yupo karibu na serikali
*Jamii inamuabudu na
*katika nyumba za ibaya yeye huwa juu na huonekana hana dhambi na anaaminika kabisa
Ila walau yeye tajiri mtenda dhambi atakavyokutana na moto mbinguni (atakua amebalance)


Ila masikini mwenye dhambi duniani atakapokutana na moto mbinguni itakua ni KASHESHE ( maskini anaenda kukutana na moto wa pili mbinguni) nadhani maskini huyu anataman hata kusiwe na uzao upya baada ya kifo (reincanation)


*Kama kuna moto mbona tayari tupo motoni*

Post a Comment

0 Comments