K’naan (KEINAN
ABDI WARSAME) ni msanii kutoka CANADA na pia ni mzaliwa wa SOMALIA mjini Mogadishu.
Watu wengi wanamtambua kwa nyimbo yake maarufu ya waving flag ambayo
aliitunga kwaajili ya kuwaamsha wananchi wa SOMALIA na harakati zao za
uhuru/ukombozi na baadae ilitumika kwenye kombe la dunia kama ilivyokuwa
kawaida ya wasanii baadhi kupata nafasi ya kutunga au kutumika nyimbo zao pale
unapofika msimu wa kombe la dunia (Ilikua south Africa 2010).
Ana nyimbo nyingi lakini tuitazame hii FATIMA, NI nyimbo inayojenga hisia
kubwa pale unapopata kutambua chanzo chake. Nyimbo hii ipo kwenye album yake ya
TROUBADOUR ambayo ilitoka mwaka 2009
ikiwa na vibao vingine kama waving flag, take a minute na people like me.
Fatima ni hadithi ya msichana mdogo na mrembo ambaye
walipendana sana na Knaan wakiwa wadogo huko Somalia (walikua ni majirani).
Knaan anasema alikua ni msichana wa ajabu ambaye alimwona ni kama alien kwakua
aliweza kuzungumza lugha tatu (Kiswahili, Kiarab na Kingereza) licha ya wote
kuwa ni wasomali na wamekua pamoja.
Kwa mikakati ya utoto, walipanga kukimbia
Mogadishu pamoja, kwakua kulikua na vita kali sana kipindi hiko na walipanga
watakimbilia Newyork Marekani pindi watakapokuwa wakubwa.
Wakati
wao wanapanga hivyo, familia ya knaan ilikua tayari kwenye mkakati wa kwenda
marekani ambapo baba yake mzazi alikua anaishi.Kwa umri wao wa miaka 12 kipindi
hiko, hawakua na la kufanya zaidi ya kuwasikiliza wazazi wao. Kabla hajaondoka
kwenda nawyork, Knaan alipatiwa barua kadhaa na FATIMA, barua ambazo aliziandika
kwa kingereza ili ampe Knaan chachu ya kujifunza kingereza haraka pindi
atakapofika Marekani.
Siku
tatu baada ya Knaan kufika marekani, alipata taarifa kuwa FATIMA ameuawa kwa
kupigwa risasi kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa inaendelea
nchini SOMALIA. Wasomali wengi waliikimbia nchi yao kwakua kulikua na vita ya
wenyewe kwa wenyewe ambayo ilianza mwaka 1986. Knaan aliondoka Somalia mwaka
1990.
Baadae
Knaan alielewa kilichoandikwa kwenye barua na rafiki yake FATIMA. Na kumpelekea
kuandika nyimbo yake hiyo na kuijumuisha kwenye album yake ya Troubadour,
ingawa nyimbo hiyo inaeleza tu jinsi alivyompenda FATIMA na kuonyesha maumivu
aliyoyapata pale alipomwacha kwenye vita huko SOMALIA. Nadhani FATIMA sio tu
nyimbo ya upendo, bali pia ni nyimbo ya kupinga vita.
0 Comments