HISTORIA MUZIKI: FELA KUTI , AFRIKA NA UAFRIKA VOL 1

Kuti ndiye muanzilishi wa mtindo wa muziki wa afrobeat uliotamba miaka ya 1970. Ambao ni mchanganyiko wa midundo ya Yoruba, Jazz, Highlife na Funk. Mpigania haki za binadamu na alitumia mziki kufikisha ujumbe wa siasa kwa jamii. Kama ni mpenzi wa muziki wa msanii Burna Boy, anafanana na mtindo wake wa muziki ni sawa na wa Kuti.

Mama yake Funmilayo Ronsome-Kuti alikuwa mpiganiaji wa haki za wanawake katika serikali ya kikoloni na baba yake Padre Israele Oludotun Ransome-Kuti, alikuwa padre, alikuwa mwalimu mkuu na alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Walimu.

Kaka zake Fela wote walikuwa madaktari mashughuri nchini Nigeria. Binamu yake Fela ni mwandishi wa kwanza wa ki-Afrika aliewahi kupata tunzo ya Nobel kwa uwandishi wake Wole Soyinka. Wengi humtambua kwa kitabu chake cha "THE LION AND THE JEWEL"

Wole Soyinka Mwandishi wa kitabu cha "THE LION AND THE JEWEL"
 

Fela alipata elimu yake katika shule ya Grammar ya Abeokuta mjini Abeokuta. Baadae alipelekwa London mwaka 1958 kusomea udaktari lakini aliamua kuacha masomo hayo na kusomea mziki Trinity College of Music, tarumbeta ikiwa kifaa alichopendelea zaidi.

Mwaka 1977, Fela na bendi yake ya Afrika ‘70 walitoa album ya Zombie, ikiwa ni shambulio kwa serikali ya Nigeria alitumia neno la zombie kuelezea mbinu za askari na wanausalama wa Nigeria. Album hii iliuzika sana na ilileta tafrani katika serikali na ilipelekea kuanza kwa shambulio la Kalakuta Republic, (hii ilikuwa Republic ilianzishwa na Fela) katika shambulio hilo maelfu ya askari walijeruhi raia. Fela alipigwa sana na mama yake ambae alikuwa mzee alirushwa dirishani, kitendo hicho kilimsababishia majeraha makubwa na baadae kifo cha mama yake.

Funmilayo Ronsome-Kuti, Mama wa Fela Kuti


Mwaka 1984, serikali ya Muhammadu Buhari ilimtia hatiani Fela kwa kosa la kutorosha fedha, kosa ambalo Amnesty International ilithibitisha kuwa ilikuwa ni mbinu za kisiasa. Amnesty iliweka kesi hii katika daraja la mfungwa wa kisiasa na ilisimamiwa na vikundi vya utetezi wa haki za binadamu. Baada ya miezi 20 jela, Fela aliruhusiwa kutoka gerezani na Generali Ibrahimu Babangida.

Mnamo tarehe 03-08-1997 Olikoye Ransome-Kuti ambae alikuwa katika mstari wa mbele katika matibabu na uelimishaji wa ugonjwa wa AIDS akiwa Waziri wa Afya, alitangaza kifo cha mdogo wake kuwa kilisababishwa na AIDS. Zaidi ya watu milioni mbili walihudhuria mazishi ya Fela.
Marehem Fela Kuti


“Hauwezi kuimba muziki wa Kiafrika kwa Kiingereza sahihi” FELA ANIKULAPO KUTI

Post a Comment

0 Comments