Josiah
Mwangi Kariuki, almaarufu kama J.M Kariuki. Mwanaharakati na mwanasiasa
na maarufu, aliyekaa gerezani kama mwanachama wa Mau Mau, kundi ambalo
lilikuwa limepigania uhuru wa Kenya mnamo 1963. Aliyechaguliwa kwenye
bunge la Kenya na kuwa mtu muhimu kwa Rais wa Kenya. Mtu mwenye chachu
ya maendeleo ambaye kukosoa kwake serikali hakukumpatia tunzo ndani ya
serikali yamzee Kenyatta, bali maadui na kifo chake.
JM Kariuki alikuwa mtu mwenye utata toka alipozaliwa mnamo 1929 hadi mwaka aliyokutana na umauti 1975.
Inadaiwa ya kwamba, alikua mcheza kamari na alilelewa akiwa motto wa pekee wa kiume kwenye famiia ya watu watano.
Alilazimika
kuacha shule kwa sababu ya kukosa ada na hapo ilimbidi aombe kazi
kwenye shamba la wakoloni ili kupata pesa. Aliishi ki mkanda mkanda hadi
hapo mwaka 1946 aliposhinda bet ya mashindano ya mbio za farasi huko
Nakuru
Akatumia fedha yake
ya bet kujiandikisha shuleni, kasha alijiunga na Mau Mau, na wakati
Kenya ilipopata uhuru, aliingia rasmi kwenye ulingo wa siasa.
Hapo
awali walikuwa marafiki wazuri na rais wa kwanza wa nchini Kenya bwana
Jomo Kenyatta, wawili hao walikosa kuelewana baada ya JM kuhoji kuhusu
wizi wa ardhi.
“Watu wetu
waliokufa msituni walikufa wakiwa na udongo katika mikono yao huku
wakiamini, wameanguka kwenye pambano kwaajili ya kurudisha ardhi yetu
... Lakini sasa zinachukuliwa na watu wachache ambao ni walafi na
wabinafsi. Lazima tufanye kitu sasa, maswali kuhusu ardhi yatajibiwa kwa
umwagaji damu. "
Haya
yalikuwa maneno ambayo JM Kariuki aliyatamka wakati alipozungumza na
kikundi cha wafuasi wake katika moja ya mkutano wake uliopigwa marufuku
mnamo 1974 kama ilivyonukuliwa katika kitabu cha Simiyu Wandiba 2001 JM
Kariuki.
Haikuchukua muda
mrefu, ekari 700 za ngano kwenye ardhi ya Kenyatta huko Rongai
zilichomwa moto na ng'ombe kuchinjwa vibaya. Huo ulikuwa mwanzo wa
mwisho kwa JM.
Mara tu
baada ya tukio hilo la kuchoma moto, ilisemekana JM Kariuki aliajiri
vijana na kuwezesha kupata mafunzo ya wapiganaji wa msituni nchini
Zambia. Chanzo cha uvumi huo pia kilidai kuwa kikundi hicho kilikuwa na
mipango au kujihusisha na mabomu.
Februari
1975 mabomu mawili yaliyopandwa huko Nairobi, yalilipuka na mtuhumiwa
number moja akawa JM. Kwasababu ya kutingwa na mawazo na matukio
yaliyomtokea kipindi hiko, daktari alipendekeza bwana JM achukue
mapumziko ya muda.
Alikuwa
na rafiki wa kike anayeitwa Elizabeth Koinange. Kwa siri walikata
tiketi ili wasafiri kuelekea Mombasa siku ya ijumaa usiku
Siku
ilipofika, Daily Nation iliripoti kwamba rafiki yake alimwambia JM
kwamba alifuatwa kwa siri na simu yake inafuatiliwa, kwa hivyo hafai
kusafiri kwenda Mombasa. Wakaghairisha safari.
Dakika chache basi la OTC ambalo alipaswa alipaswa kusafiri nalo kutokea Nairobi lililipuka na kuwauwa abiria 27.
Nyakati
za mwisho akiwa hai, alikuwa katika Hoteli ya Hilton, masaa 48 baadaye,
alifuatana na walinzi wa Kenyatta, mnamo Machi 2, 1975. Inasemekana
alikua na cheki ya dola 340 siku hiyo, pesa aliyokuwa ameikusanya.
Watu
wasiojulikana kuwa ni majambazi au polisi waliingia hotelini na
kumchukua JM moja kwa moja mpaka kwenye gari nyeupe na kamanda wa GSU
Ben Gethi akishuhudia tukio hilo.Huku gari hilo likifuatwa na magari
mengine manne.
Mwili wake
ulipatikana kwenye barabara ya Ziwa Magadi, mwili wake ukiwa umechomwa.
kifo chake kilipokelewa kwa hasira kubwa nchini Kenya. Mwili ulipelekwa
mochwari ukiwa unatambulika kama mwili usiojulikana wa jambazi wa
kijaluo.
Baadae
mwili huo ulitambulika na mke wake ambaye alipewa taarifa na mtu
asiyejulikana kuwa akautazame mwili wa mume wake mochwari.
Alijua
mume wake hayupo nyumbani. Na alisisitiza kuwa mume wake alijua kuwa
anafuatiliwa. Alipomshauri atembee na walinzi alimjibu “ hakuna wa
kunizingua”
1 March Mrs
Kairuki alimpeleka mume wake hospitali kwaajili ya maumivu ya mguu.
Waliachana huko huko hospitali na Mrs Kairuki kurudi nyumbani.
Kabla
JM hajapotea, aliacha ujumbe kwa wafanyakazi wenzake kuwa anatoka
kuonana na Ben Gethi, jamaa wa usalama ambaye alimuita siku hiyo
asubuhi.
Mke
wa tatu wa JM alipoona mume wake haonekani, alitoa taarifa kwa familia
nzima. Na kuamua kuuliza serikalini JM yupo wapi. Jibu walilopatiwa ni
kwamba JM ameelekea Zambia mara moja.
Familia
ilishtushwa na suala hilo kwakua passport yake ya kusafiria alikua
ameiacha nyumbani. Ujumbe wa mwisho mke wake huyo ni ya kufika mjini
Nairobi ili kuona mwili wa mume wake kipenzi.
Mke
wake aliripoti kuwa. Sura ya mume wake ilibadilika na kuwa nyeusi, kana
kwamba kuna kitu alimwagiwa usoni. Huku mguuni mwake akiwa ameandikwa
mtu asiyetambulika. Ilimuuma kwakua alijua mume wake ni maarufu Kenya
nzima.
12 March, afrisa wa polisi alithibitisha kuwa mwili wa Kariuki ulikuwa na majeraha mawili ya risasi.
Ripoti
ya hospitali ilisema uso wa JM ulikua mweusi kama alivyoona mke wake
kwasababu ya acid aliyomwagiwa ikiwa na dhumuni la kufanya asitambulike.
Wanafunzi
wa Nairobi waliandamana kwakuona hali ya Kenya ni mbaya. Akiwa kama
mwanasiasa na mwanaharakati wa tatu kuuawa ndani ya miaka 10.
Serikali
iliruhusu uchunguzi kufanyika. Lakini kabla report haijatolewa, raisi
Kenyatta aliamrisha baadhi ya majina yafutwe. Wengi walisema majina hayo
alikua na ukaribu nayo.
0 Comments