TwitReporter/HumphreyMoris |
Leo nimeona nisambaze Link ya mfano wa jarida ambalo nimekua nalitengeneza AFRIKA NA UAFRIKA na nimekua nikituma story kwa mfumo wa thread kwenye TL yangu. Kuna story chache kama 20 tu lakini kazi bado inaendelea. Na Huyu ni mimi na hii ni kama blurb.
Twitreporter
jina kamili Humphrey Moris ni mtayarishaji, Mtangazaji na Mwandishi wa habari
kutoka Tanzania. Huripoti matukio kupitia Mitandao ya kijamii na hasa mtandao
wa twitter pamoja na blog yake binafsi.
Pia
ni mwalimu wa mtandaoni ambae hufundisha masuala ya teknolojia kama vile (Matumizi
ya kawaida ya kompyuta, Simu, Graphics designing:Picha na video ) Mtayarishaji
wa video na vipindi mbalimbali vya televisheni, redio pamoja na Makala.
Mhitimu
wa shahada ya mawasiliano ya umma na uandishi wa habari katika chuo kikuu cha
mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Mwaka 2019.
Nimekua
nikijihusisha na uandishi wa habari wa mtandaoni kuanzia mwaka 2016 mpaka sasa.
Na nimekua mpenzi sana wa masuala ya kijamii pamoja na historia kwa kipindi
chote cha maisha yangu. Hii imenipelekea kuanzisha aina ya jarida lenye dhumuni
la kuelezea matukio na historia mbalimbali kutoka barani afrika. Na kulipa
jarida hilo jina la AFRIKA NA UAFRIKA.
Jarida
hili linarushwa mtandaoni bure kabisa. Document iliyotimia na kuwa na visa au
matukio zaidi ya 10 huwekwa mtandaoni ili wapenzi wa jarida wapakue na kusoma
kwa utulivu. Lakini pia matukio haya hutumwa kwenye akaunti yangu ya twitter
(kwa siku habari moja). Nikiwa na lengo la kuwafanya watu wajitambue na
kufungua minyororo ya utumwa wa kifikra kwa kushuhudia wengi na mengi bila
kusahau yaliyofanywa mazuri na muhimu ili wote tuige au kuyaishi. Na pia ni
sehemu ya chakula cha ubongo, kwamaana msomaji anaingiza kitu kipya kichwani
mwake. Ninaweka mtandaoni nikiwa na dhumuni la kuyajadii pia yale
ninayoyaandika na watu mbalimbali kwakua ni njia rahisi kupokea ushauri na
maoni.
Sijawa
na bajeti kubwa ambayo ingenisaidia kutembelea sehemu nyingi na kuandika yale
ninayosimuliwa kwa kuona, kupiga picture na kutengeneza kitu kikubwa kilichojitosheleza
zaidi ya hiki ninachokifanya. Kwa uwezo wangu mdogo ninakusanya taarifa zangu
kupitia vitabu/simulizi na mitandao ya kijamii. Hakuna data hata moja mpaka
sasa ambayo nimetumia mawazo yangu pekeangu.
Kazi
ya kuunda jarida nimefanya kwa mikono yangu, picture nyingi ni za mtandaoni
pamoja na taarifa baadhi.
SHUKRANI ZA DHATI kwa wote wanaofuatilia kazi zangu na kutosita
kunishauri au kunikosoa. Pia kwa wote wanaonisaidia kusambaza ( mfano ku
retweet) kwasababu sina uwezo wa kufikishia watu wengi taarifa hizi. Hivyo
nategemea wasomaji wangu au watu wenye wafuasi wengi kuniinua,
Mkono
wangu na ufundi wa kutengeneza jarida hili
ni zao imara la mwalimu wangu Elisha magolanga
Kichwa
changu ni zao la vingi na mengi akiwemo mwalimu Richard Mabala, ni mtu wa
kwanza ambaye ana jina kubwa kupenda nilichoandika mtandaoni na nnakumbuka siku
hiyo alinifollow back japo sidhani kama anakumbuka.
Bila
kusahau uandishi wangu ni zao kamili la Denis Mpagaze.
JARIDA NI BURE
LAKINI
KAMA UTAWEZA KUNICHANGIA KWENYE HARAKATI
ZANGU UNAWEZA NISAIDIA CHOCHOTE KUPITIA NAMBA ZANGU ZA SIMU
+255625773039 AU +255742965664.
NAPOKEA
MAONI NA USHAURI, KIELIMU NI MTAALAMU WA MAWASILIANO YA UMMA HIVYO NINAWEZA
WASILIANA NA MTU YOYOTE NA AKAFURAHI AU AKAPATA KITU ALICHOHITAJI KUTOKA KWANGU.
NAPATIKANA MASAA 24
0 Comments