HISTORIA: PROF WANGARI MAATHAI , AFRIKA NA UAFRIKA VOL 1

Mwanaharakati mashuhuri wa mazingira na haki za binadamu kutoka nchini Kenya.
mwanamke wa kwanza katikati au mashariki mwa Afrika kushikilia Ph.D., mwanamke wa kwanza wa idara ya chuo kikuu nchini Kenya.



Katika kipindi cha robo karne, alithubutu kupambana na utawala wa rais Daniel Arap Moi, wakati wanasiasa wa kiume wa nchi hiyo wakikubali kughilibiwa na kuchezewa shere na rais huyo, utawala wa Rais Moi ulimtupa gerezani mara kadhaa.
Katika miaka ya tisini alisimama kidete kupinga kujengwa jengo la ghorofa sitini katika Uwanja wa Mapumziko wa Uhuru Park, katikati ya mji wa Nairobi. 


Bibi Maathai aliuliza kwanini tunakuwa na mbuga za hifadhi kwa ajili ya vifaru na tembo, lakini hatutaki kuwa na uwanja wa kupumzikia kwa ajili ya wanadamu?
Mume wake, aliyezaa naye watoto watatu, licha ya kwamba alikuwa katika siasa, aliziona harakati za mke wake zinakwenda mbali mno, hivyo wakachana.

Maathai alikuwa mashuhuri kote duniani na alipanda miti popote alipozuru.
Mbali ya kuwa Mwanaharakati wa Maswala ya Mazingira na haki za binadamu , Wangari Maathai pia alikuwa mwanasiasa shupavu. 


Amewahi kuhudumu kama Mbunge na Naibu waziri wa Mazingira nchini Kenya.
Prof Maathai pia katika uhai wake alipata tuzo mbalimbali za kimataifa kwa kutambua mchango wake.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004 na kuwa mwanamke wa kwanza mwafrika, mkenya wa kwanza na mwanamazingira wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo.


Mnamo mwaka 2007 Prof Maathai alijiwekea historia ya kuwa mwanamke wa kwanza Afrika na mwanamke wa nne duniani kupata tuzo ya Indira Gandhi Price. Tunzo hizo utolewa kwa watu au taasisi ambayo imefanya ubunifu wa kuendeleza mazingira na maendeleo ya nchi kwa ujumla.


Mwaka 2011 Prof. Wangari Maathai alifariki baada ya kuugua Ugonjwa wa Kansa ya mfumo wa uzazi (Ovarian cancer). Mazishi ya masiba wake ulifanyika mjini Nairobi

“Fursa zipo hata kama ni kipindi kigumu” Prof. Wangari Maathai

Post a Comment

0 Comments