Alizaliwa, akapambana na kuuliwa
kikatili, tofauti na wengine, yeye hata nchi yake ilipanga kufutilia mbali
historia yake na kumtambua. Marehem akumbukwe kwa mazuri bwana. Hata
anapopumzika ajiskie kweli alifanya kitu. Hii ni imani yangu mimi muafrika, kama
hyukubali pole sana.
Awamu mbili za utawala wa mwanzo wa Kenya baada ya uhuru,
ile ya Mzee Jomo Kenyatta na baadaye wa mrithi wake, Daniel arap Moi, zilikataa
kumtambua na kumpa Kimathi heshima ya kuwa mpiganiaji uhuru, zikimuangalia kama
gaidi. Ndiomaana nikasema hata baada ya kifo chake walitaka kumpuuza.
Lakini baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na
kuingia madarakani kwa Rais Mwai Kibaki hapo mwaka 2006, serikali ilimtangaza
Kimathi kuwa ni shujaa wa vita. Na mimi namuunga mkono Kibaki.
Alipofika umri wa miaka 15, alijiunga
na shule ya msingi kijijini kwao, Karuna-ini, ambako alijifunza Kiingereza kwa
ufasaha na kuitumia lugha hiyo baadaye kuandika mengi kabla na baada ya uasi wa
Mau Mau. Alishiriki sana katika mijadala shuleni na alikuwa na kipaji cha
kuandika mashairi. Mimi Kuanzia leo nampa jina la Dedan Makengeza.
Alijiunga na jeshi la uingereza
lakini alifukuzwa kwa madai ya utovu wa nidham. Na hapo akaenda kwenye ualimu
lakini alikosa kazi pia baada ya muda. Akagundua bado waafrika au Kenya haipo
huru na kuingia rasmi msituni mwaka 1951 ambapo akajiunga na wapiganaji wa mau
mau
Aliteuliwa
kuwa katibu Mkuu wa wapiganaji hao katika tawi la Thomson Fall na kusimamia
nidhamu kwa wanajeshi wa maumau. Inasemekana alisimamia viapo kwa wapiganaji
hao na hata kutumia vitisho ili wanajeshi hao wakae kwenye mstari imara. Maana
kwenye mapambano msaliti mmoja anaweza kusababisha matatizo kwa kikosi kizima.
Hivyo Dedan aliwapika wapambanaji kisawasawa.
Mwaka
wa 1951 alikamatwa na Wakoloni lakini askari weusi waliokuwa ndani ya kikosi
cha usalama walimsaidia kutoroka.
Mwaka 1953, Kimathi akaunda
Baraza la Ulinzi kuratibu shughuli za wapiganaji wote wa msituni.
Mwaka 1956, miaka minne
tangu kuanza uasi huo, Kimathi alikamatwa katika misitu ya Nyeri na kundi
lililoongozwa na Ian Henderson. Kukamatwa kwake kukawa mwisho wa vita vya
msituni. Walikata mizizi mti wote ukaanguka lakini mapambano hayo yalikua
chachu ya ukombozi na uhuru wa wakenya.
Alihukumiwa
kifo na Jaji Mkuu O`Connor huku akiwa kitandani hospitali kuu mjini Nyeri. Alinyongwa
mapema asubuhi ya tarehe 18 feb 1957 katika gereza kuu la Kimiti.
Mahala
alipozikwa hadi leo hapajulikani.Juhudi nyingi zimefanyika ili kupata kaburi la
Dedan. Kuna baadhi ya chapisho zilisema kaburi lake limepatikana lakini taarifa
hiyo ilikanushwa.
Kimathi anaangaliwa kama shujaa wa taifa na
serikali ya sasa na kuna sanamu maalum la "Mpigania Uhuru Dedan
Kimathi" katikati ya jiji la Nairobi, lililozinduliwa tarehe 11 Desemba
2006, katika kumbukumbu ya tarehe aliyouwawa.
“Siongozi
magaidi. Ninaongoza Waafrika ambao wanataka serikali yao binafsi na ardhi.
Mungu hakukusudia kwamba taifa moja litawaliwe na mwingine milele. “
0 Comments