Hii sio AFRIKA NA UAFRIKA... leo nakusimulia kuhusu paka aliyenusurika kufa vitani mara tatu.
Paka
ana roho ngapi???.... utaskia watoto wanajibu ANA ROHO SABA Labda
theory hii ya kikatili ya kumsifu paka ana roho saba ilianza kwa paka
OSCAR. Kwenda JKT tu kwa vijana sasa ni mbinde. Kuna njemba moja siitaji
jina ilisema ni heri asiende chuo kikuu kuliko kwenda JKT kwa mujibu.
Vijana hawana moyo kama ule wa enzi za vita vya kagera.
Labda paka huyu atawapa ujasiri ndugu zangu
Oscar
AKA UNSINKABLE SAM… ni jina la utani la paka wa kwenye meli za kivita
,ambaye alishiriki wakati wa Vita vya Kidunia vya pili na kwa bahati
aliwahi kuishi pande mbili za maadui. Mwanzo aliishi kwenye meli ya
Kriegsmarine ambayo ilikua chini ya jeshi la ujerumani na baadae kwenye
meli za jeshi la uingereza (Royal Navy) na alinusurika kuzama kwa meli
zaidi ya mara tatu.
Jina
la asili la paka huyu halikujulikana ila aliitwa jina la OSCAR na
wafanyakazi wa meli ya uingereza ya HMS Cossack meli ambayo ilimuokoa
kutoka baharini kufuatia kuzama kwa meli ya Ujerumani Bismarck. Meli
ambayo ilipewa jina la kiongozi wa wakati huo Otto Von Bismack
"Oscar"
ilitokana na ishara ya wanajeshi wakiwa vitani, pale mtu anavyotaka
kuzama majini hutumia neno O wakimaanisha man overboard ili uweze pata
msaada wa kuokolewa
Bismarck
Paka
huyo mwenye rangi nyeusi na nyeupe alikua anamilikiwa na mtu ambaye
hakujulikana katika meli ya Bismarck. Ilikuwa safarini mnamo Mei 18,
1941. Meli hiyo ilizamishwa baada ya vita kali ya baharini mnamo Mei 27,
vita ambayo ilipigwa baina ya Bismarck na The Prince of Wales. Meli iliharibiwa vibaya na haikuweza kukarabatiwa.
Watu
115 tu ndio walinusurika kati ya watu 2,100. Masaa kadhaa baadaye,
Oscar alikutwa akielea juu ya maji na meli ya HMS Cossack. Walimwokoa na
hapo ndipo alipohama upande wa ujerumani na kuwa upande wa Uingereza na
kupewa jina jipya la OSCAR
HMS Cossack
Paka
huyo aliishi kwenye meli ya Cossack kwa miezi michache baadae wakati
meli ilipokuwa ikifanya majukumu ya kusindikiza wanajeshi na vikosi
vingine kwenye Bahari ya Mediterania na kaskazini mwa Bahari ya
Atlantiki. Mnamo tarehe 24 Oktoba 1941, Siku moja Cossack ilikuwa
akisafirisha msafara kutoka Gibraltar na ndipo ilipo haribiwa vibaya na
meli ya ujerumani U-563. Kikosi kikahamishwa kwenye HMS LEGION na
kufanyika jaribio la kuirudisha meli iliyoshambuliwa huko Gibraltar.
Lakini hali mbaya ya hewa iliwafanya waitelekeze meli hiyo. Siku moja
baadae Cossack ilizama ikielekea magharibi mwa Gibraltar.
Mlipuko
wa awali ulikuwa umesababisha theluthi moja ya sehemu ya mbele ya meli
hiyo kuvunjwa vunjwa vibaya na shambulizi lilipelekea vifo vya watu
159, lakini paka Oscar alikutwa kwa mara ya pili akielea juu ya maji na
kurudishwa salama huko Gibraltar. Maofisa wa jeshi la uingereza walimpa
jina jipya la Unsinkable Sam kwa kutozama majini wakati wa vita kwa mara
ya pili. Visanga havikuishia hapa, bado OSCA tunamkuta kwenye
mapambano.
OSCAR
akakaribishwa kwenye meli aina ya HMS Ark Royal meli ambayo ilikuwepo
hata siku BISMARCK ilipozama. Na sasa imepewa jina jipya la “lucky ship”
meli yenye bahati. Bahati haikufika mbali ikawa meli yenye gundu na
balaa. Mnamo 14 Novemba 1941 meli hii pia iliangushwa
Walionusurika,
pamoja na Sam, ambaye alikuwa amepatikana akielea kwenye mabaki ya vitu
vilivyoharibiwa. Inasemekana alikua mwenye hasira sana wakati huo labda
kwakua aipoteza marafiki, me sijui. Nisimwongelee paka wa watu. Labda
alihitaji pensheni yake.
Alihamishiwa
na safari hii alirudi kufanya kazi nchi kavu akiwa kama mwindaji wa
panya katika ofisi za Gavraltar na kisha akarudishwa Uingereza. Picha ya
zamani ya Sam (iliyopewa jina la Oscar, paka wa Bismarck) na msanii
Georgina Shaw-Baker iko katika Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya huko
Greenwich.
Baadhi ya viongozi wanahoji ikiwa wasifu wa Oskar / Sam unaweza kuwa "hadithi tu ya baharini.
0 Comments