Mchawi
mpatie mwanao amlee, kauli ina ukakasi hii. Ndio hatomuua, lakini je
akimfundisha uchawi mtoto huyo na kuja kuwa balaa kwenye nyumba yako?.
Kuna wachawi wameokoa watu na kupata tuzo. Wenzetu wa kabila Fulani
wakikuhisi tu hata kama una macho mekundu wanakuua. Tumepoteza mashujaa
wengi sana. Hii sio movie, maana usijedhania nataka kukusimulia hadithi
za Merlin kwenye nchi ya Camelot.
Huu
ni mkasa wa kweli kuhusu bibi Zura Karuhimbi. Mwanamke aliyeweza kuokoa
mamia ya watu katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994
Zura
Karuhimbi hakuwa na silaha yeyote ya kujilinda wakati wanaume waliokuwa
na silaha walipoizunguka nyumba yake na kumtaka awakabidhi watu
aliokuwa amewahifadhi nyumbani mwake.
Mwanamke huyo alikuwa anajulikana kuwa na nguvu za giza.
Hali
iliyowafanya kundi hilo la wauaji kuwa na uoga na kumfanya mwanamke
huyo mzee kuwaokoa watu zaidi ya 100 kuwa salama wakati wa mauaji ya
kimbari nchini Rwanda.
Vyumba
viwili vidogo vilivyopo kijijini Musamo, kwa haraka vilikuwa sehemu
salama kwa watusi, Waburundi na hata wazungu watatu walijificha humo
wakati wa mauaji ya kimbari.
Makundi ya watu yaliripotiwa kuwa walikuwa wamejificha chini ya kitanda na eneo lingine la siri juu ya paa.
Huku wengine walisema kuwa alikuwa amewachimbia shimo kuwaficha.
Baadhi yao walikuwa watoto ambao walichukuliwa kutoka kwa mama zao waliokufa, alisema hivyo.
Karuhimbi
alimwambia mwandishi wa habari wa Rwanda Jean Pierre Bucyensenge katika
kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari kuwa ,
“Silaha pekee ya Zura ilikuwa ni kuwatisha wauaji kuwa atawaloga wao pamoja na familia zao, “ bwana Bucyensenge alieleza
Maisha
yaliendelea huku akiwa ni mwanamke ambaye anaomboleza kupotea kwa mtoto
wake katika vurugu hizo na binti yake ilijulikana kuwa aliwekewa sumu
akafa.
Pamoja na umaarufu mkubwa alioupata kuwa alikuwa mchawi lakini hakuwa mchawi na wala hakuwahi kuwa mchawi.
Mwaka
2006, bibi huyo alitunukiwa tuzo ya kupambana na mauaji ya kimbari na
rais wa Rwanda Paul Kagame, Tuzo ambayo alikua analala nayo kitandani
siku zote . Tuzo hiyo ilimpa nafasi ya kusimulia namna alivyookoa watu
wengine 50 katika miaka ya nyuma. Aliweza kumwokoa kijana wa kitutsi
miaka ya 1950. Wahutu waliua watoto wa kiume wa kitutsi, bibi huyu
alimsaidia mwanamke mmoja aliyebeba mtoto wa kiume kwa kumfunga shanga
kichwani ili wauwaji hao wamdhanie ni motto wa kiume.
Na
ilimsaidia motto Yule kuokoka kwenye mikono ya wanyamera. Bibi Zura
alimfananisha motto Yule na Rais wa Rwanda Paul Kagame. Na kusema,
nimemsaidia Kagame ambaye leo hii amenipatia tuzo. Hii ikimaanisha bibi
Yule alikua akiamini katika Karma ( wazungu wanasema goes around comes
around) kitisho cha uchawi chaokoa mamia nchini Rwanda.
kama watakufa basi na mimi pia nitakufa, Hata kama ningejua mtuhumiwa yeyote , nisingeweza kumzuia.”
0 Comments