CHAMBUZI KUHUSU AFRIKA NA KIFO CHA GEORGE FLOYD

By HumphreyMoris

Watanzania na waafrika wanapinga tukio la Askari kusababisha kifo cha Mmarekani George Floyd. Wamarekani wameandamana huku waafrika/watanzania wakitoa maneno makali mitandaoni na mitaani juu ya tukio hilo.

Kwangu mimi kifo au ukatili ule umenifunza kuwa umma ukiamua kupata mabadiliko lazma wayapate, umma una nguvu kuliko kitu chochote na tumeona jinsi gani demokrasia ilivyo kwenye nchi kama marekani (Fikiria waandamanaji wa Tanzania au nchi za Afrika wangekua wamekufa wangapi hadi mda huu?) nimesema fikiria, sijatoa takwimu ni mawazo tu.

Pia nimeona nguvu ya media, shkamoo media na tutaliangalia hili pia kidogo


Umma unalilia haki ya Floyd, niongeze kwa kusema umma wa wamerekani na dunia kwa ujumla unamlilia Floyd (aibu kubwa) sio aibu kumlilia bali kifo chake kilichotokana na kitendo cha kinyama. Sikatazi waafrika au watanzania kulaani kitendo kile. Ila tujiangalie na sisi matukio ya mauwaji ni mengi Afrika.
Matabaka juu na chini, mavazi makazi duni ahsante Nikki Mbish kwa somo japo wengi hawafuatilii na kujadili mawaidha mazuri kama haya. Mbona tuna matatizo mengi Afrika na hatulalamiki na wala hatusaidiwi kulalamika na upande wowote, najua sababu ni sisi wenyewe kuwa kimya.

Amepigwa Boby wine tumekaa kimya

Alitishwa Nape bunduki tumekaa kimya.

Aliuawa Daud Mwangosi tukakaa kimya
Amepotea Azory tumekaa kimya
Alitekwa na kusulubiwa ulimboka tukakaa kimya
Ameuawa Akwelina tumekaa kimya
Ameuawa Alphonce Mawazo tumekaa kimya.


Wengine ndo kwanza hawajulikani hata wamefariki vipi, utapata majibu ya kuhisihisi ukiangalia historia yao ya nyuma kabla ya kifo, pumzika Stan Katabalo, Ben saa nane na wengine. Wacha tulie na kupeana matusi mitandaoni kwa kifo cha Floyd huko marekani.

Tungesimama na kupinga hili, pande zote duniani labda wangeungana na sisi kupambana na kudai haki. Tumeona jinsi wazungu walivyoungana na watu weusi kupinga manyanyaso yale, hii ni nzuri sana. Kwetu vyama tu havipatani, hawa wakipigwa wengine wanafurahi,hawa wakitekwa na kuteswa hawa wanafurahi, KWANINI?
KWANINI WAAFRIKA TUSIUNGANE KWENYE MATESO KAMA HAYA?, tunajisahau sana, tunasahau kuwa umoja unaweza leta haki kwa wote na tukapendana kama wanavyoungana leo wazungu na waafrika kutaka watu weusi wapate haki yao kama wanavyopata watu wengi huko Marekani.

Tumelitolea macho tatizo la marekani na kusahau majanga yetu waafrika. Usininukuu vibaya, ni jambo zuri ila je wakati unamtoa mwenzako kibanzi jichoni, hiyo boriti kwenye jicho lako umeitoa??, mind ur own business mzee kabla hujavamia za watu, yako yanakushinda kazi kuchunguza ya wenzako, ahsanteni kwa kijembe hiki (Sheki na Avil), wasanii waliimba bwana.

Nikupe elimu moja
jambo ambalo watu kama Mustapha Masmoud kutoka Tunisia na mwalimu Nyerere waliungana na viongozi wengi wa Afrika miaka ya 1970 mwishoni walilipinga sana. Ni kuhusu media zinavyofanya kazi na utofauti mkubwa kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Sio twitter na mitandao ya kijamii tu, namaanisha hata redio, tv pamoja na magazeti.
Habari tunazozipata ni nyingi kuliko zinazotoka.

Na habari yetu inayotoka kutoka Afrika ni lazma iwe mbaya ili ipate soko kwenye nchi za ulaya.


Kilio hiki cha waafrika kilipelekea Rais wa marekani wakati huo Ronald Reagan pamoja na waziri mkuu wa uingereza Margaret Thatcher kujitoa UNESCO, Kwasababu ya viongoz wa Afrika kuwatuhumu kwenye suala la media (kureport, aina ya matangazo na aina za habari) Tusilale sana kwenye hili, ila lichukue na upate kujua mengi kwa kujiongeza mwenyewe.
Turudi kwa Floyd na mfumo wa media za Afrika na marekani. Juzi tu Burkinafaso wameuawa watu 35 kwa siku mbili mfululizo. Si Tanzania wala nchi zingine za Afrika hatujui kinachoendelea kwa jirani zetu wa afrika

Mfumo wa vyombo vya habari umekua kama theory ya hub na spokes katika tairi la baiskeli
yani habari ya marekani inafika moja kwa moja Tanzania kuliko habari ya nchini Uganda ambayo ni nchi ya karibu na sisi.
Hii spoku ni hatari sana
Hii ndio sababu macho ya dunia nzima yameelekezwa chini Marekani, unadhani hakuna yanayoendelea Afrika?_ japo watu wa nje wapo vizuri kwenye kushare mabaya ya Afrika , kuna wakati wanakua kimya (huu ni ule wakati ambao tuna uhitaji wa kuyatambua) Na pengine sio kosa lao, ni kosa letu wenyewe Waafrika kutojiweka karibu na kutambua yanayotusibu, tupo busy kufuatilia na kutukana mitandaoni kwa ubaya aliofanyiwa Floyd na kusahau yote yanayotusibu kila siku.

Tuna kina Floyd wengi Afrika, wengine wamesahaulika na nnaamini wanalia huko walipozikwa kwa kuwaona waafrika wenzao wakipayuka ya wenzao na kusahau ya kwao. Mimi sio mbaguzi na usiseme nambagua mweusi mwenzangu, ila fikiria yanayokusibu kabla hujaungana na majirani kuangalia yanayowasibu, japo tunajua serikali na viongozi wetu ni chanzo cha sisi kuwa kimya, tumefungwa minyororo na kutolewa meno chonge yote. pumzika kwa amani George Floyd, kifo chako kiwe chachu ya ukomboz kwa waafrika, tukimaliza 40 ya floyd naomba tuje tupambane na ya kwetu sasa


Post a Comment

0 Comments