MK-ULTRA: MKAKATI WA UCHUNGUZI WA C.I.A NA KIFO CHA JOHN LENON (MWANAMUZIKI KIKUNDI CHA THE BEATLES)

KIFO CHA JOHN LENON 8 December 1980


Watu waliotumika kufanya mauwaji ya watu wakubwa , wengi wao ukiwafuatilia wanakua walipata mafunzo ya kijeshi. Au mafunzo na kufanyiwa unyama huu wa Mk-ultra. Kama umetazama movie za James Bond au Jason Bourne USIDHANI yameisha kwenye movie tu, haya mambo yapo. Mtu anatekeleza mauaji kwa kutumwa na hata jina lake halijui (yeye mwenyewe hajijui jina). Anaishi kama robot na amesahau kila kitu. Anaweza kukuua nayeye kujiua au kuuawa baada ya muda Fulani. Hawa watu hufanya walichotumwa, na huwa hawafanyi makosa.


Kunataarifa zinasema,aliyekuwa Mwanamziki mashuhuri wa kundi la the beatles “John Lennon” aliuawa na C.I.A baada ya kuonekana ana itikadi za kikomunist na harakati zake za siasa.

John Potash mwandishi wa Drugs as Weapons Against Us, anasema: Lennon alikua anafuatiliwa muda mrefu na C.I.A kwasababu ya harakati zake.

Taarifa za siri zinasema, Lennon alianza kufuatiliwa toka miaka ya 1970 baada ya kujitangaza ameachana na madawa ya kulevya, na kuanza kutoa elimu juu ya athari ya dawa hizi. Kumbuka C.I.A ndio walihusika kutangaza madawa kwa mikakati yao ambayo utaiona hapo mbele. Hivyo wakamwona Lennon ni tishio .


Album ya Lennon Some Time in New York City ni album iliyojaa siasa na harakati aliimba kuhusu Black Panthers, haki za wanawake na haki za waingereza wenye asili ya marekani. Lennon aliuawa mwezi mmoja baada ya kua raia kamili wa Marekani.

Kitendo cha Lennon kuachana na dawa za kulevya kiliwakera sana C.I.A (utadhani kama natania vile)

Mwandishi Phil Strongman, kwenye kitabu chake cha John Lennon: Life, Times and Assassination, ANASEMA Chapman (MUUWAJI WA LENNON) Alishikwa akili yake (MK-ULTRA) Ili amuue John Lennon. Utajionea pia kuhusu Mk-Ultra.

Watu walihoji kwanini CHAPMAN anaonekana kama roboti?


Katika mazungumzo na mwandishi Bresler,Afande kutoka New York Arthur O’Connor alisema, hivyo ndivyo anavyoongea na ndivyo alivyozaliwa.

Hapo ni miaka ya 1980 na inasemekana mkakati wa Mk-Ultra ulishapigwa marufuku toka 1973, je ni kweli?????? Me ngoja niishie hapa kwa Lennon, Twende kwenye unyama huku



Mk-ultra


Mkakati haram ulioandaliwa na shirika la C.I.A kwa dhumuni la kupata taarifa za siri za binadam kwa kuishika akili yake. Kushika akili namaanisha kufanya kitu au kuongea kitu bila kudhamiria. Sawa na mtu aliyetumia vilevi na ubongo wake kuhama kimawazo. Mtu kama huyu ukimpatia bunduki ajiue ni dakika moja tu anamaliza kazi. Utaona kama movie vile, ila hii kitu ni kweli na inasadikika njia hii inatumika mpaka sasa, japo walikiri kuisha kutumika miaka ya 1973.


Kwa maelezo ni kwamba,Mwaka 1953 Allan Dulles,mkurugenzi wa C.I.A aliidhinisha mkakati huu Kufanyika toka miaka hiyo mpaka miaka ya 1970, hapa siri ndipo zilipovuja. Kama unakumbuka miaka hii mambo hayakua mazuri kidogo kwenye uongozi wa marekani na mashirika yake ya usalama.

Lengo la kuanzisha Mk-ultra ilikua ni kupambana na maadui ya kisovieti, yani wale woooote walioonekana kuwa na akili ya kikomyunist. Hivyo walitaka kutumia mpango huu kuwatambua maadui na wapelelezi wa kikomyunist. Tambua marekani iliogopa watu wenye akili ya kijamaa kuliko inavyoogopa korea kwa sasa. Urusi na china wamewatesa sana marekani.


Marekani waliamini wanajeshi kama kamikaze kutoka Japan na wanajeshi wa NAZI hawakua na akili ya kawaida. Walikua watiifu na hata ukiwaambia wajilipue ni sekunde tu wanafanya hivyo. Hivyo waliamini ile ni mind control kwasababu hata wafungwa wa kivita wa Marekani, walirudi nyumbani wakiwa akili zao zipo tofauti kidogo, wanaamini nao walifanyiwa hiki kitu huko Urusi, china, korea ya kaskazini na kambi ya Dachau concentration camp iliyopo ujerumani kwa nyakati tofauti tofauti.
Na wao wakatafuta njia ya kushika akili za watu. Ila njia yao ilikua ya moto kidogo

Mk-Ultra ilifanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo… kutumia madawa makali ya kulevya kama ilivyo LSD, Hii dawa ukimeza inakufanya uwe mwepesi kufanya unachoambiwa kukifanya, pia inakufanya uone mawenge na hudumu mwilini kwa saa 12 Kama itatumika kawaida.


Dawa za kulevya zilifanyiwa majaribio hasa kwa wanawake wanaojiuza, na watu wa mitaani. Walifungiwa nyumba moja (nyumba zilizomilikiwa na C.I.A) WANAWAPA MADAWA na kutega camera ili kuona matukio yalivyokua yakifanyika humo ndani. Zile dawa zilikua zinawarusha akili. Mpaka sasa dawa hizi zinatumika.

Kando na dawa za kulevya, tiba ya electroshock na hypnosis pia zilitumika kuwapa watu hofu, wasiwasi na hata kufuta kumbukumbu. Walitumia "mbinu ambazo zitakandamiza akili ya mwanadamu hadi ikakubali chochote".

Wakidhamiria usahau kila kitu, ndani ya mwezi mmoja utafundishwa hadi kuvaa nguo na viatu. Utakua umesahau kila kitu. Na utakua umesema kila kitu.

Electroshock hii ni shoti ambayo inapigwa kichwani kwa lengo la kucheza na sehemu za ubongo. Huwa inatumika zaidi kwa wagonjwa wa akili. Wao walifanya kwa watu wazima kwaajili ya kupata wanachohitaji.

Majaribio kabla hawajaanza kutumia njia hizi haram yalifanyika kwenye kambi za siri mno. Ilihusisha majaribio kwa binadamu zaidi ya 150, HAWA NDIO WALIOFAHAMIKA, kwasababu data nyingi zinazohusu Mk-ultra zilifutwa kwaajili ya kupoteza ushahidi. Walikua wanawajaribu hasa vyuoni, hospitali na jela (jamani jela kuna mambo, kila baya linaenda huko)

Wanafunzi walidhani wanafanya utafiti na kujikuta wamefanyiwa wao utafiti bila kujua.

Post a Comment

0 Comments