Kuna hadithi tatu zinazozunguka juu ya kile
kilichotokea kwa majivu ya Tupac, kama hautambui ni kwamba, Baada ya
kifo cha Tupac alichomwa moto ikiwa kama destruri ya watu wengi. kupenda
kufanyiwa hivyo au hata familia kuamua.
Simulizi Mbili zinaaminika kabisa na ya mwisho ina ukakasi kidogo.
Wacha tuanze na hii yenye mashaka kidogo.
Kikundi
cha mziki cha Tupac kinachojulikana kama OUTLAW wanadai walichanganya
majivu ya tupac na sigara ( sijui ni sigara kubwa au ndogo) na kuyavuta.
Lakini hakuna mwanachama wa kikundi anayeonekana kukubaliana ni wakati
gani na mahali ambapo waliyavuta majivu hayo. Hii inaleta ukakasi
kuamini kama ni kweli walifanya hivyo . Kwenye nyimbo yao kikundi cha
OUTLAWS inayojulikana kama Black Jesus, dakika ya 2 sekunde ya 15 tupac
anatoa husia kwa rafki zake kuwa baada ya kifo achomwe moto na majivu
yake yavutwe kama sigara.
Hiyo
story imekaa juu juu sana, japo kuna wanaoamini kuwa ni kweli
walichanganya majivu yake na vileo mbalimbali na kuvuta. Kwa chanzo cha
kuaminika zaidi, mama wa Tupac ambaye naye ni marehemu, Afeni Shakur.
Siku moja baada ya Tupac kufariki, alichomwa moto, na kukabidhiwa majivu
yake.
Baadae
Afeni alisema kwamba alieneza majivu ya mwanaye mahali Fulani huko Los
Angeles na pia alichukua majivu yaliyobaki na kurudi nayo nyumbani kwake
huko Stone Mountain, Georgia. Na huko alieneza majivu yaliyobaki katika
bustani yake.
Simulizi
ya tatu kwa mara nyingine inatoka kwa mama wa Tupac Afeni Shakur. Na
simulizi hii inahusiana na kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Tupac,
mnamo 2006. Ni kwamba Afeni Shakur alichukua majivu ya mtoto wake na
kwenda nayo Soweto huko Afrika Kusini.
kulingana
na maelezo yake SOWETO S.A ndio "MAHALI WALIPOZALIWA BABU ZAKE KI
HISTORIA". Pia anasema Soweto ndio mahali yalipozaliwa mapigano ya
demokrasia na kupinga ubaguzi wa rangi yaani Apartheid, mfumo wa
kikatili ambao ulitekelezwa na makaburu huko South Afrika", Afeni
alishawishika na tabia ya mwanae Tupac ya kusimama imara kama mtetezi wa
haki za watu weusi. Kuna mipango mingine inayohusiana na ziara ya Afeni
nchini Afrika Kusini, kama vile ujenzi wa makumbusho huko Soweto kwa
kuheshimu mziki na harakati za Tupac, ambayo itakua ni sehemu ya jumba
la kumbukumbu ya muziki na sanaa nchini Afrika Kusini. Alisema: "Matukio
yaliyotokea [Soweto] ni sehemu ya historia yetu na itakuwa heshima kwa
mwanangu kupumzika mahali hapa maalum".
0 Comments