Joker
au jokeri, wacheza karata wanampenda na wanamwogopa, akikulalia huyu
unahesabiwa una 50, kwenye adhabu unamlambisha mtu 5. Tuachane na huyu
Joker
anayejulikana kwa jina la Arthur Fleck (jina halisi Joaquin Phoenix)
kupitia movie ya JOKER 2019 na movie zingine nyingi zinazomuonyesha kuwa
mpinzani mkubwa wa Batman kwa miaka 80 sasa tunasimuliwa stori zake.
Flexk
anaonekana kupambana na ugonjwa wa akili, ugonjwa unaomfanya asipendwe
na kila mtu. Kihistoria anaonekana anabaguliwa toka akiwa mdogo mpaka
anakua mtu mzima. Ana ugonjwa wa kucheka, yani jamaa anaweza kucheka
hadi akatokwa na machozi,
mpaka
alikua anatembea na karatasi ili akianza kucheka anakupatia mtu wa
karibu yake usije kumwona mdwanzi. Kikaratasi kinakuambia samahani, nina
ugonjwa wa kucheka naomba unisamehe, hapo hata kukuambia kwa mdomo
anakua hawezi
Movie ya
JOKER haikusema ni ugonjwa gani Fleck alikua anaumwa, lakini kitaalamu
wanasema huu ugonjwa wa kushinwa kujizuia kucheka unaitwa Pseudobulbar
Affect kwa kifupi PBA Hali hiyo husababisha kucheka kicheko kisichoweza
kudhibitiwa au hata kulia,
na
kawaida hutokea kwa watu ambao wana Multiple sclerosis (MS) na
amyotrophic lateral sclerosis (ALS) (matatizo katika neva au majeraha
kwenye ubongo) Wataalam wa afya watatusaidia kwenye hili
Phoenix
AKA Fleck aliwahi kusema, nafasi aliyoicheza amewawakilisha wale wote
wanao/waliochekwa wakiwa mashuleni, mitaani- kwaajili tu ya kuwa tofauti
na watu wengine (Mwonekano, ulemavu) na kukosa sehemu ya kufikisha
matatizo yao. Kisaikolojia inaweza mfanya mtu kuwa mhalifu.
0 Comments