Kwasasa
imekua lugha inayotumika kwenye mambo maalumu tu, je kuna ubaya
nikisema hii lugha imekufa?, kama ulikua hujui kuwa lugha inakufa ndo
ujue leo, wataalam wa lugha wanaweza kuelezea lugha inakufa vipi.
kama
ni mfuatiliaji mzuri wa historia, najua haukuwepo ila unatambua jinsi
utawala wa warumi ulivyokua na nguvu kabla hata ya ujio wa yesu, enzi za
kina kaisari na Cleopatra. Nikukumbushe tu Malkia Ckeopatra wa Egypt
alimzidi yesu miaka 69
Lugha
yao ilikua kilatini. Baba wa ufalme wa roma alikua Romulus na iliyemfia
Roma aliitwa Romulus Augustus, tawala ilijengwa na kubomolewa na
Romulus (unampatia mtoto jina kudhani atakuwa na bahati kama mwenye
jina, kumbe ni nuksi tupu). Sitambui ni kitu gani hasa kilipelekea
utawala wa waroma kuanguka na hiyo haikua sababu ya lugha ya kilatini
kupotea kwasababu ilizidi kuwa hai zaidi ya miaka 500
karne
ya 5 baada ya kuzaliwa Yesu, roma ilishikwa na wajerumani. Wavamizi
zaidi ya makabila ma 5 ya kijerumani yaliishika Roma kinguvu. Kila
kabila lilizungumza Lugha yake. Chakushangaza baada ya muda fulani,
wavamizi wote walikua wanazungumza kilatini. Bwana awe nanyi
Mimi
na wewe tujiulize, je lugha mama (kingereza Orijino kabisa, kwasasa
sidhani kama kina mzungumzaji) ambacho kimezaa lahaja mbalimbali tena
nyingi na chenyewe kubadilika kwa misamiati mipya ndio kufa huko?
Tofauti
ya kilatini na kingereza ni kwamba, karne ya 6 baada ya utawala wa
warumi kuanguka ndipo lugha hii ilianza kupata kashikashi. Lahaja
mbalimbali ziliibuka na kuchota lugha ya kilatini, lahaja hizo za warumi
zilikua ni Kifaransa, kireno, kiitaliano, kispanish (kihispaniola) na
kiromania. Kiitaliano na kiromania hufanana kwa kiasi kikubwa na hivyo
wazungumzaji wanaweza kuelewana. Japo lugha hizo zote 5 zinaingiliana
kidogo. Wenyewe huziita lahaja za kirumi (romance language / dialects)
Hivyo
watu waliacha kabisa kuandika na kutumia kilatini na kuanza kucheza na
lugha hizo tano. Hivyo kusema kilatini kimekufa ni sawa na kusema
kingereza halisi kimekufa kwakua hakina mzungumzaji. Japo ni ngumu
kukiita kilatini kiitaliano cha zamani loooh mambo haya si mchezo,
kilatini huitwa hivyo hivyo latin.
Tunasema kilatini kimekufa, lakini kwanini kimekuwepo kwa muda mrefu hivi? watu wanajifunza kilatini hadi leo hii
Kulitokea
dini ndogo ambayo ilitukanwa sana, na watu wa pembeni waliita dini ya
mungu maskini. Maadui wa dini hii waliita dini ya kikristo
(christianity) japo wenyewe walijiita KANISA (ECCLESIA). Wakristo wa
kwanza walikua wayahudi na kanisa lilianzia kwenye masinagogi (nyumba ya
ibada) wakiwa wanasambaza ujumbe wa ukombozi kwa ulimwengu. Wakati
utawala wa roma unaanguka, dini ya kikristo ndipo ilipokua inazidi
kupata nguvu. Kumbuka roma ilianguka karne ya 5. Ila hadi kufika karne
ya 6 hima iliyodondoka ilikua na wakristo wa kutosha. Hadi kufikia karne
ya 7, dini hii ilishaanza kuenea kwenye maeneo mbalimbali.
Jerome
ambaye inasemekana alikua padri wakati huo alikua anazungumza sana
kilatin, kigiriki na kihebrania, alipewa kazi ya kuchapisha biblia na
Papa Damasus mwishoni mwa karne ya 4 kabla roma haijaanguka. Kwa miongo
miwili huu ndio ulikua mkakati mkubwa wa kanisa. Japo chapisho la Jerome
halikua chapisho la kwanza la kilatin, yalikua mengi na yalisambaa
sehemu nyingi. Kwakua wakristo ni watu wa vitabu, lugha ya kilatin
ilienea kabla hawajaanza kutafsiri lugha hiyo kwenda kwenye lugha
mbalimbali za watawala wapya. Gothic (jamii ya watu Fulani ya wajerumani
ambao ndio wavamizi wa mwanzoni huko Roma) walikua watu wa mwanzo
mwanzo kutafsiri biblia kwenda kwenye lugha yao.
Ndio
maana Lugha ya kilatini ni lugha official inayotumika kwenye kanisa la
Roma. Ukitembelea Mji wa Vatikan, utaona bado wakatoliki wanachapisha
nakala zao kwa lugha ya kilatin.
kutokea
na kukua kwa dini ya kikristu ni chanzo cha lugha ya kilatini kutumika
kwenye mambo kadhaa mpaka leo hii. Baadhi wanajifunza na mafunzo kadhaa
ambayo ni mazuri (sayansi etc) yapo katika lugha ya kilatin.
Je
lugha inaweza kufufuka? na kuwa imara upya?? na kupata wazungumzaji
ambao watakua watumiaji wa kwanza wa lugha hiyo (lugha mama)??
0 Comments