Nampenda Jay kwasababu anaimba na kuandika maisha yake halisi.
Ukisikiliza
nyimbo yake ya You Must Love Me na Kill jayz, amewahi kutaja kisa cha
kumpiga risasi kaka yake, akiwa na umri wa miaka 12. Walipitia maisha
magumu na familia yake na ni msimu ambao hata baba yake aliitelekeza
familia.
Kaka wa Jay Z,
Erick alikua mraibu (addict) wa dawa za kulevya. Jay alimwona kaka yake
kama anaongeza mzigo kwenye familia, kwasababu maisha yalikua magumu na
bado alikua anaiba vitu ndani, siku aliyompiga risasi alikua ameiba pete
ya Jay. Bahati nzuri kaka alipona na kumsamehe mdogo wake. Jay alikiri
kupagawa na kuhisi angeishia jela, na alimpiga risasi kaka yake ili
WANAFAMILIA wamwone kuwa anaweza kuijali familia yake. Aliwahi kuulizwa
kama amewahi kuua maishani mwake, alikataa na kusema HATA KAMA INGEKUA
KWELI, ASINGESEMA
Alipoulizwa , bunduki ya kumpiga kaka yake aliitoa wapi? alijibu " Niliiba nyumba ya jirani"
Tuachane na hili
Tuje
kwenye album ya 4.4.4, hii album Jay ni kama alimtungia Beyonce
hahahahaaa (natania, ila ameimba mengi kuhusu familia/ndoa yake). Hivi
unajua kwanini Jay Z anaitwa elevator punching bag? Majanga yalianza
mwaka 2014 ambapo Bwana Jay Z alipigwa na shemeji yake Solange (Mdogo wa
Beyonce). Video clip ilivuja kutoka mtandao wa tmz, ikionyesha jinsi
jayz anavyoshambuliwa na shemeji yake kwenye lift hotelini. Beyonce
alikua pembeni na hakujitikisa hata kidogo. Haikujulikana sababu ni nin.
Mwaka
2016, Beyonce alitoa album ya Lemonade na katika kibao chake cha sorry,
alimpiga vijembe mume wake kwa kusema, “ananihitaji anaponimis” “ila
mara zote hufurahi akiwa na Becky Yule mdada mwenye Nywele nzuri”. Kila
mtu aliuliza huyo Becky ndio nani? Mambo yalionekana sio mazuri kwenye
ndoa ya Jay na Beyonce (ambao walifunga ndoa ya siri mwaka 2008)
Ghafla
baada ya nyimbo ya sorry ya Beyonce kukick na kusambaa kwa yale maneno
ya Becky. Mwanamitindo Rachel Roy ambaye aliwahi kuwa msimamizi wa
biashara za nguo za jay z (ROCKAWEAR) Toka miaka ya 1996, alipost
instagram picture akiwa anajibu maneno ya Beyonce kuhusu Becky mwenye
nywele nzuri, na kiukweli Rachel Roy ni mwanadada mwenye nywele nzuri na
huzitunza nywele zake, hivyo baada ya ile post, watu walitia sahihi
kuwa Becky with good hair ni Rachel Roy.
Baadae
ilionekana ndio sababu ya Solange (Mdogo wa Beyonce) mwaka 2014,
kumvamia Jay Z kwenye lift huku dada yake akiwa anatazama bila kusaidia
chochote. Na kabla ya hapa inasemekana walianza kugombana na Roy
(BECKY).
Mwaka 2017 ambapo
Jay Z alitoa album ya 4:44, alikiri kumcheat Beyonce na kusema
“nilimlaumu Solange kwa kusema alifanya utoto, ila kwakweli nilimkosea”.
Na Kukiri ule ndio mtiti pekee uliowahi kutokea baina yake na mke wake,
waliamua kukaa chini na kuyamaliza. (aligusia machache kwenye nyimbo ya
KILL JAY Z)
Album
ya 4:44 ilikua ni sehemu ya majuto na kukiri makosa yake huku bila
kusita amekua ameomba msamaha live na kwa siri mara nyingine.
Family
Feud na video yake inaongea bila vificho na anamtaja Becky amwache na
familia yake/asije kumuharibia "Yeah, I'll f*ck up a good thing if you
let me/Let me alone, Becky. A man that don't take care of his family
can't be rich."
Kill Jayz, amezungumzia kisa chake na Solange kwenye Lift na kuwataka wanaume wote wasiende nje ya ndoa (You egged Solange on
Knowin' all along, all you had to say you was wrong
You almost went Eric Benét
Let the baddest girl in the world get away
I don't even know what else to say
Nigga, never go Eric Benét)
Never go Eric Benet anawataka watu wasiwe waraubu kwa nje ya ndoa kama yaliyowahi kumkuta Eric Benet)
0 Comments