Wajibu na Sera

Ni wajibu wa mtu kutekeleza kile anachoahidi. Wananchi wanaweza kupendezwa na unachoahidi au kukizungumza . Kwa mfano ; wananchi wanaweza kupendezwa na sera za kibaguzi hivyo wakikiteua ufanye ubaguzi kweli kwakua walikipenda hiko.
Wananchi wanaweza kupendezwa na sera za mauwaji , basi ukiingia madarakani ua kweli kweli kwakua wananchi ndio walichokupendea na kukushikisha hatam na usifanye tofauti na ahadi zako (Tekeleza) kwakua wengi walikupendea hiko au walizidi kukupenda kwaajili ya hiko.
Na pia sio mbaya kwa kiongozi kuendeleza kile alichofanya mwenzake.

Nawapongeza marais wote wa Tanzania kwa kutekeleza vizuri sera zao na kwa upeo wangu mdogo nimejaribu kuziangalia hapa.

1:Hayati Mwalimu J.K. Nyerere
Uhuru na kazi
uhuru tulikua nao na kazi ilifanywa kweli kweli si mchezo. Kila rika lilichapa kazi japo nchi ilikua changa. Nakumbuka baadhi ya nyimbo zikiwa zinaelezea nidhamu ya kazi.

Ucwe kupe jtegemee,mengi yanaishi mpaka leo. Watanzania waliacha kuwa kupe na kuanza kujitegemea hasa katika sekta ya kilimo. Nchi ilianza kutoka kwenye uchanga.

uchumi unaukalia, ulipo ndipo kwenye fursa. kwa asilimia kubwa rasilimali yetu ilikua ni kilimo hivyo wengi walishika jembe na kulima. Watu hawakukalia tena uchumi. Viongozi nao waliwajibika kutoa misaada kwa wananchi wahitaji

siasa ya ujamaa na kujtegemea, mwalimu aliitekeleza sera hii na hakuna atakaye pinga. Tanzania tulikua wajamaa haswa na baadhi ya sehem nchini kwetu watu wanaishi kijamaa mpaka leo na hata waliopo mijini, ujamaa bado upo damuni mwetu kwakua mwalimu alirithisha hili suala kwa sera na utelekezaji wa kweli. Leo Mkurya na mmakonde wanaishi pamoja . Pongezi kwa hayati mwalimu
Sera zingine ni kama elimu haina mwisho,kisomo chenye manufaa,umoja ninguvu utengano ni udhaifu,klimo ndyo uti Wa mgongo

2:Ally Hassan Mwinyi
Mzee mwingi aliingia na sera ya soko huria na kupewa jina mzee wa ruksa. Wananchi walinufaika sana kwakua mipaka ya kibiashara haikua migumu tena vitu vingi vilienda na bila kusahau sera ya mwalimu nyerere ya Uhuru

3: Benjamin Mkapa.. Alipambana na ufisadi na kumuunga mkono Mwalimu J.K.Nyerere.
Sera ya soko huru kama ilivyo kwa Mzee mwinyi na kubinafsisha makampuni yanayomilikiwa na serikali na kupelekea baadhi ya madeni nje ya Tanzania kufutwa
pia kilikua ni kipindi cha UKWELI NA UWAZI...Hapa wasanii kama kina profesa J waliimba sana nyimbo za kuonyesha mfumo wa maisha ya wana siasa wanavyofanya (ahad na kutotimiza)
..waandishi waliandika sana
...wananchi waliongea na kutoa maoni yao ,vijana wanaita kuchana (watu walichanana kisawa sawa) bila kusahau kua mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe

4:Rais Jakaya Kikwete
Hali mpya nguvu na kasi
licha ya kuwepo kwa kauli mpya lakini mzee aliendeleza ya wenzake na kwa asilimia kubwa alisimamia kauli yake na wenzake pia
..wasanii walifanya kaz zao na wenye kukosoa walikosoa ILA HAKUACHA KUWA RAFIKI , alipenda kutabasamu na kutumia wakosoaji wa mazuri kama njia ya mafanikio kwake

5:Rais John Magufuli
Hapa kazi tu
Hapa kazi tu na nnakuachia msomaji ufanye kazi ya kuchambua mwenyewe kwakua hapa kazi tu

na nnakuachia ufanye kazi kwakua mrisho mpoto anasema KUKU ANAYETAGA HACHINJWI ... mimi nitachambua na kunyambua siku ya mwisho baada ya kumaliza mda japo uelekeo unaweza kuonyesha mambo fulani kwa asilimia fulani na wazungu wanasema *smell premiditate deliciousness* yaani harufu inaashiria utam
kama harufu ni nzuri bhas hata utam utakua uzuri kabisa ila kama harufu ni mbaya utam utakua sio utam tena.

Post a Comment

0 Comments