Na Loveness Daniel
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mh.Hassan Ngoma amezindua rasmi zoezi la utoaji chanjo ya matone kwaajili ya kudhibiti ugonjwa wa kupooza (polio) leo tarehe 1 September 2022.
Utoaji wa chanjo ya matone ya polio katika Halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa ni kampeni inayoendelea kwa awamu ya tatu ya utoaji chanjo hiyo muhimu inayotolewa nchini Kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ambayo itafanyika Kwa siku 4 kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 4 september mwaka huu 2022.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imepokea dozi 22,240 ya chanjo ya polio ikiwa na lengo la kuwafikia walengwa 22,926.
Hata hivyo mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Dkt.Salvio wikes amewaomba wananchi kuendelea kupokea elimu zinapotolewa na wahudumu wa afya wanapofika kliniki pia kutoa ushirikiano wakati wa ufanyikaji wa huduma tembezi ya chanjo ya matone ya polio.
Dkt.wikes amesema katika awamu ya pili ya utoaji chanjo ya polio Wilayani Ruangwa ilifanikiwa Kwa 117% ikiwa zaidi ya watoto 22,926 walipata chanjo huku Halmashauri ilikua na lengo la kuchanja watoto 19,654.
Mnamo tarehe 18Mei 2022 zoezi chanjo ya polio iliizinduliwa rasmi wilayani ruangwa na mkuu wa wilaya Mh. Hassan Ngoma huku Halmashauri ikipokea chanjo dozi 24,160 na kusambazwa kwenye vituo 40 vya kutolea huduma.
Polio ni ugonjwa wa kupooza Kwa watoto /ugonjwa wa kuambukiza wa mfumo mkuu wa Neva unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalamu kama poliomyelitis.
0 Comments